Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli: Mwakyembe alinyweshwa sumu
Habari za Siasa

Magufuli: Mwakyembe alinyweshwa sumu

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema, Dk. Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela alinyweshwa sumu kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akiwa Kyela mkoani Mbeya leo tarehe 30 Aprili 2019 kwenye ziara yake ya siku nane, Rais Mgufuli amesema kuwa, sababu ya Dk. Mwakyembe kunyweshwa sumu na hata kupelekwa kutibiwa nje ya nchi ni kutokana na kusimamia haki.

“Mheshimiwa Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu (Naibu Waziri wa Ujenzi), alinisumbua sana na hili nasema wazi, amewahi kunyweshwa sumu, akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki.

“Inawezekana nyinyi watu wa Kyela hamumjua vizuri Mwakyembe, sikuja kumpigia kampeni lakini nina haki ya kusema ukweli kwa sababu ukweli utakuwa ukweli tu,” amesema Rais Mgufuli.

Taarifa kwamba, Dk. Harrison mgonjwa na kuwa alinyweshwa sumu zilizagaa mwaka 2011, wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Kwa kipindi chote hicho, si serikali ama familia ya Dk. Mwakyembe iliyoweka wazi ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Dk Mwakyembe alikumbwa na ugonjwa wa mnyauko uliopukutisha ngozi yake hadi kufanya sura yake ya awali kutoweka.

Tuhuma zilielekezwa kwamba, Dk. Mwakyembe amenyweshwa sumu na maofisa ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Kutokana na tuhuma kusambaa kwa kasi kwamba, baadhi ya maofisa serikali walitumika kupanga mpango na hata kufanikiwa kumnywesha sumu Dk. Mwakyembe, Jeshi la Polisi lilikana madai hayo.

Mwaka 2012, Robert Manumba, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wakati huo, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kwamba, polisi ina uhakika kuwa, ugonjwa wa Dk. Mwakyembe haukutokana na kulishwa sumu.

Kauli ya Manumba ililenga moja kwa moja kukanusha madai ya Marehemu Samuel Sitta, aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki kwamba, ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ulitokana na kulishwa sumu.

Kauli kwamba Dk. Mwakyembe alinyweshwa sumu, ilisimamiwa na Sitta kwa zaidi ya miezi sita tangua kuanza kuumwa kwake. Dk. Mwakyembe alitibiwa India.

Chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kilidaiwa kuwa, ni maji aliyonawa ofisini kwake na baadaye kujipanguza kwenye kitambaa kilichokuwa maliwatoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!