January 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ateua wabunge 2

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS Tanzania, John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Rais Magufuli amemteua Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Katika Bunge la 11 lililomalizika, Riziki alikuwa mbunge wa viti Maalum kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye mwishoni mwa Bunge hilo, alitangaza kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikuku imesema, wabunge wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

error: Content is protected !!