March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli aonya wanaovujisha siri za Serikali, kujipiga ‘selfie’

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amewaagiza wateule wake kutotumia mitandao ya kijamii katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Maagizo hayo ameyatoa leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020 mara baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri 21 na manaibu waziri 23, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Mawaziri hao aliwateua tarehe 5 Desemba 2020.

Rais Magufuli ameagiza wateule wake kutotuma nyaraka za serikali kwa kutumia mitandao ya kijamii, badala yake watumie njia za barua.

Amesema baadhi ya mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya wana tabia ya kutuma nyaraka zao katika makundi ya ‘WhatsApp’ hali inayosababisha siri za Serikali kuvuja.

“Sababu ndani ya Serikali sasa hivi kuna ugonjwa mmoja, hata mawasiliano yanatumwa kwenye ma-group (kundi), barua nyingine ni za siri.”

“Utakuta makatibu wana andikiana hivyo au mawaziri, makatibu wakuu na ndio maana siri kwenye Serikali zinavuja. Governament goes on paper (Serikali inaendeshwa kwa karatasi),” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amewataka wateule wake kutofanya kazi zao kwa maonesho, akisema kwamba anayefanya kazi anajulikana hata kama asipojitangaza mitandaoni.

“Lakini sitaki ule muonekano wa kisasa gari inateremka kwenye mteremeko unaji-Salfie (kupiga picha), unasema unavyoniona hivi naondoka na gari langu naenda kukagua mradi, hayo yamepitwa na wakati, ukifanya kazi utajulikana tu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka wateule wake na watumishi wa umma kusimamia maadili ya viapo vyao.

“Kwenye mambo ya Serikali lazima mzingatie maadili ya viapo vyenu na hili sizungumzi kwa mawaziri tu,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu mawaziri aliowaapisha, amewataka wasiwe wazito katika kufanya maamuzi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

“Ndio maana nawaomba makafanye maamuzi, ni vizuri ufanye maamuzi mabaya kuliko kutokufanya uamuzi, narudia ni nafuu ukafanaye uamuzi mbaya kuliko kutokufanya uamuzi,” amesema

“Kafanye uamuzi hasa uamuzi unaohusu maslahi ya Taifa, utakaosaidia kuoko shida za wanyonge vijijini, naamini nimechagua watu watakao kwenda kufanya maamuzi sababu nawaaamini mkafane kazi kweli,” ameagiza Rais Magufuli.

Mwaziri walioapishwa ni, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Jumaa Aweso, Waziri wa Maji na naibu wake Maryprisca Mahundi; Kapteni mstaafu, George Mkuchika wa Utawala Bora na naibu wake, Ndejembi John.

Wiliam Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na naibu wake, Angelina Mabula; Innocent Bashungwa wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na naibu wake, Abdallah Ulega.

Jenista Mhagama wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu na manaibu wake, Ummy Nderiananga atakayeshughulikia Watu Weenye Ulemavu na Patrobas Katambi wa Kazi, Ajira na Vijana.

Profesa Kitila Mkumbo wa Uwekezaji); Dk. Mwigulu Nchemba wa Katiba na Sheria) na Naibu wake, Gefrey Pinda.

Mashimba Ndaki wa Mifungo na Uvuvi na naibu wake; Pauline Gekul, Dk. Damas Ndumbaro wa Maliasili na Utalii na Naibu wake, Mary Masanja; Selemani Jaffo wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi na manaibu wake, Dk. Festo Lugange na David Silinde.

Dk. Medard Kamelani wa Nishati na naibu wake, Stephen Byabato; Profesa Adolf Mkenda wa Kilimo na naibu wake, Husein Bashe; Doto Biteko wa Madini na naibu wake, Francis Ndulane.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema atafanya uteuzi wa naibu mwingine badala ya Ndulane ambaye ameshindwa kuapa vizuri kiapo chake.

George Simbachawene wa Mambo ya Ndani na naibu wake, Hamis Hamza Hamis

Ummy Mwalimu wa Muungano na Mazingira na naibu wake, Mwita Waitara; Dk. Faustine Ndugulile wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na naibu wake, Kundo Mathew.

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na naibu wake, Dk. Godwin Mollel

Wengine ni; Dk. Leonard Chamriho wa Ujenzi na Uchukuzi na naibu wake, Msongwe Kasekenya; Geofrey Mwambe wa Viwanda na Biashara) na naibu wake, Kigahe Silaoneka.

Profesa Joyce Ndalichako ameapishwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na naibu wake, Kipanga Omary.

Manaibu wengine waliapishwa leo ambao mawziri wao waliteuliwa awali, ni Mwanaidi Ali Hamis wa Fedha na Mipango na William Ole Nasha wa Mambo ya Nje.

Mawaziri wa wizara hizo, Dk. Philip Mpango wa Fedha na Mipango na Profesa Palamagamba Kabudi wa Mambo ya Nje, walikwisha apishwa.

error: Content is protected !!