Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli amwambia Makonda “chapa kazi”
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli amwambia Makonda “chapa kazi”

John Magufuli, Rais wa Tanzania (kulia) akiwa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Spread the love

RAIS John Magufuli amemwambia Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, “endelea kuchapa kazi” na anamtaka aamini kuwa ni yeye rais anayepanga, wala sio kushauriwa na mtu yeyote, anaandika Pendo Omary.

Makonda amekuwa katika kipindi cha kukabiliwa na tuhuma nzito za kumiliki vyeti vinavyotajwa kuwa vimetokana na jina la mtu mwingine aitwae Paul Christian, aliyefaulu mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari ya Pamba, jijini Mwanza.

Isitoshe, Ijumaa ya wiki iliyopita, alijiongezea mzigo wa kashfa alipofuatana na polisi wenye silaha kiasi cha saa 5 usiku na kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media, kilichopo Mikocheni, na kutaka kulazimisha kurushwa kipindi cha SHILAWADU kwa namna atakavyo.

Bila ya shaka, Rais Magufuli kwa kutambua yote hayo, na kwa vile ameamua kuendelea kumkingia kifua mteule wake huyo kwa kuwa hajaamua kumbadilisha, ndani ya tuhuma hizo, leo asubuhi ametoa tamko hilo akisema kuwa “kama kuandikwa kwenye mitandao na magazetini, hata mimi naandikwa, kwa hiyo nijiuzulu?”

“Suala la kuandikwa sio tija kwangu… tunapoteza muda. Sipangiwi cha kufanya, mimi najiamini hata fomu ya kugombea urais nilichukua peke yangu sikushauriwa na mtu,” amesema wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa makutano ya barabara eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Makutano hayo yanakutanisha barabara kuu ya Morogoro kuunganishwa na Mandela inayotokea Bandari ya Dar es Salaam na Sam Nujoma inayoishia Mwenge. Ujenzi huo ni sehemu ya mradi mkubwa unaofadhiliwa kwa njia ya mkopo na Benki ya Dunia (WB).

Ujenzi huo utahusu barabara ya urefu wa kilomita moja kutoka makutano ya Ubungo kwa kila upande wa barabara hizo kuu zinazopitia makutano ya Ubungo. Ni mradi unaogharimu Sh. 188 bilioni; Benki ya Dunia ikichangia Sh. 186.72 bilioni kwa njia ya mkopo, wakati Sh. 1.96 bilioni zikitolewa na serikali ya Tanzania. Mradi utatekelezwa na kampuni ya China ambayo haikutajwa lakini muda wake ni miezi 30.

Rais wa Benki ya Dunia, Dk. Jim Yong, alihudhuria hafla hiyo na baadaye kuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli, Ikulu ya Magogoni.

Katika hafla hiyo pia alikuwepo Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, aliyechaguliwa Novemba mwaka jana kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); na Rais Magufuli alimtambua akisema anampongeza kwa ushirikiano unaojali maendeleo ya nchi ambayo ndio wananchi wanayotumaini kutoka kwa viongozi wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!