January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amuapisha waziri mkuu, mawaziri 2

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemuapisha, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Majaliwa ameapishwa leo Jumatatu tarehe 16 Novemba 2020, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Majaliwa ameapishwa kuendelea kushika wadhifa huo aliokuwa nao katika miaka mitano iliyopita ya utawala wa miaka mitano iliyipita ya Rais Magufuli.

Majaliwa alithibitishwa na wabunge wote 350 waliohudhulia kikao cha tatu mkutano wa kwanza Bunge la 12 Alhamisi ya 2 Novemba 2020 sawa na asilimia 100.

Pia, Rais Magufuli amewaapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dk. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Profesa Kabudi na Dk. Mpango waliteuliwa hivi karibuni kuwa mawaziri wa wizara hizo waliozkuwa wakiziongoza awali kabla ya utawala wa miaka mitano ya awali ya Rais Magufuli kumalizika tarehe 5 Novemba 2020 na kuanza mingine mitano siku hiyohiyo.

Wote walioapishwa, wamekula kiapo cha maadili kwa viongozi wa umma, kilichosimamiwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Harold Nsekela.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!