Magufuli amponza ‘mlevi’

HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu.

Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake.

Kesi hiyo itatajwa tena  mahakamani hapo tarehe 14 Aprili  mwaka huu.

 

HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi. Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam. Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu. Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake. Kesi hiyo itatajwa tena  mahakamani hapo tarehe 14 Aprili …

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube