RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amempongeza Dk. Lazarus Chakwera kuwa Rais mpya wa Malawi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Chakwera amechaguliwa na Wamalawi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 23 Juni 2020 kwa kupata asilimia 58 akimshinda Rais aliyekuwa madarakani Peter Mutharika.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya ule wa awali wa Mei 2019 kufutwa na mahakama Februari 2020 baada ya kubaini ulikuwa na dosari.
Soma zaidi:-
Dk. Chakwera aliwasilisha maombi hayo mahakamani yaliyompa ushindi na katika uchaguzi wa marudio, aliwakilisha vyama zaidi ya vitano vya upinzani vilivyomng’oa Mutharika.
Tarehe 28 Juni 2020, Dk. Chakwera aliapishwa kuwa Rais wa Malawi.
Leo Jumatano tarehe 1 Julai 2020, Rais Magufuli ametumiw akaunti yake ya kijamii ya Twitter kumpingeza Rais Chakwera.
Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii.
Hongera sana Mhe. Rais.— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) July 1, 2020
Rais Magufuli amesema, “Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi.”
“Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote, naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii. Hongera sana Mhe. Rais,” amesema.
Leave a comment