Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli aapisha timu yake ya mawaziri 
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli aapisha timu yake ya mawaziri 

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri na manaibu waziri aliowateua tarehe 5 Desemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Uapisho huo umefanyika leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, ikiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Pia Rais Magufuli amewakabidhi mwongozo wa Baraza la Mawaziri.

Mwaziri walioapishwa ni, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

https://www.youtube.com/watch?v=KH3_fm-82Nc

Jumaa Aweso, Waziri wa Maji na naibu wake Maryprisca Mahundi; Kapteni mstaafu, George Mkuchika wa Utawala Bora na naibu wake, Ndejembi John.

Wiliam Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na naibu wake, Angelina Mabula; Innocent Bashungwa wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na naibu wake, Abdallah Ulega.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Muungano na Mazingira

Jenista Mhagama wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu na manaibu wake, Ummy Nderiananga atakayeshughulikia Watu Weenye Ulemavu na Patrobas Katambi wa Kazi, Ajira na Vijana.

Profesa Kitila Mkumbo wa Uwekezaji); Dk. Mwigulu Nchemba wa Katiba na Sheria) na Naibu wake, Gefrey Pinda.

Mashimba Ndaki wa Mifungo na Uvuvi na naibu wake; Pauline Gekul, Dk. Damas Ndumbaro wa Maliasili na Utalii na Naibu wake, Mary Masanja; Selemani Jaffo wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi na manaibu wake, Dk. Festo Lugange na David Silinde.

Dk. Medard Kamelani wa Nishati na naibu wake, Stephen Byabato; Profesa Adolf Mkenda wa Kilimo na naibu wake, Husein Bashe; Doto Biteko wa Madini na naibu wake, Ndulane Kumba.

Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira

George Simbachawene wa Mambo ya Ndani na naibu wake, Hamis Hamza Hamis.

Ummy Mwalimu wa Muungano na Mazingira na naibu wake, Mwita Waitara; Dk. Faustine Ndugulile  wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na naibu wake, Kundo Mathew.

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na naibu wake, Dk. Godwin Mollel.

Wengine ni; Dk. Leonard Chamriho wa Ujenzi na Uchukuzi na naibu wake, Msongwe Kasekenya; Geofrey Mwambe wa Viwanda na Biashara) na naibu wake, Kigahe Silaoneka.

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria

Profesa Joyce Ndalichako ameapishwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na naibu wake, Kipanga Omary.

Manaibu wengine waliapishwa leo ambao mawziri wao waliteuliwa awali, ni Mwanaidi Ali Hamis wa Fedha na Mipango na William Ole Nasha wa Mambo ya Nje.

Mawaziri wa wizara hizo, Dk. Philip Mpango wa Fedha na Mipango na Profesa Palamagamba Kabudi wa Mambo ya Nje, walikwisha apishwa. 

Endelea kufuatili MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbaliz

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!