Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Magereza watoa elimu ya matofali ya kuchoma, kuepusha mazingira
Habari Mchanganyiko

Magereza watoa elimu ya matofali ya kuchoma, kuepusha mazingira

Spread the love

ILI kuepuka kufanya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti hovyo, Jeshi la Magereza limeitaka jamii kujifunza njia mbadala ya ufyatuaji matofali ya kuchoma kupitia pumba zinazotoka kwenye mpunga. Anaripoti Danson Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalisemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania (CPG), Phaustine Kasike wakati alipotembelea mradi wa Ujenzi wa nyumba za bei nafuu unaofanywa na nguvu kazi ya wafungwa katika gereza la Isanga na Msalato yaliyopo jijini hapa.

Kamishna Jenerali Kasike alisema ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa nyumba za wafanyakazi wa Jeshi hilo wamebuni Ujenzi wa nyumba za bei nafuu kupitia matofali ya kuchoma na ya kawaida ili kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za wafanyakazi wa jeshi hilo.

Kamishna Jenerali Kasike alisema wao kama jeshi ambalo lipo kwa ajili ya kurekebisha tabia, wamekuwa wakitekekeza agizo hilo kupitia nguvu kazi ya wafungwa kwa mujibu wa sheria kufyatua tofali hizo lakini kwa njia ya kuzichoma kupitia pumba za mpunga jambo ambalo haliathiri mazingira yanayowazunguka kwa sababu wanatumia pumba kuzichoma hadi kukamilika tofauti na ilivyozoeleka wengi wao wamekuwa wakitumia kuni kuchoma tofali hizo.

“Tofali hizi ni imara na zinatumika katika ujenzi wa nyumba ambazo wamebuni ili kupunguza gharama ya ujenzi wa nyumba hizo kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli,” alisema Jenerali Kasike.

Alisema zoezi la ujenzi wa nyumba hizo kupitia matofali ya kuchoma ni rahisi sana kwa sababu zinatengenezwa kupitia njia hiyo mbadala ya kutumia pumba badala ya kuni kitendo ambacho ni rahisi hata jamii kuitumia ili kuepusha kuharibu mazingira lakini pia zitawapunguzia gharama za Ujenzi wa nyumba za makazi.

Kutokana na hilo alisema jamii inapaswa kujifunza kupitia jeshi hilo jinsi ya njia mbadala ya kuchoma tofali hizo jambo ambalo litawarahishia kupata tofali ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi mbalimbali wa nyumba zao za makazi.

Akizungumzia kuhusiana na teknolojia hiyo mpya alisema ni moja ya ubunifu ambao unafanywa na jeshi hilo sio kwa Dodoma pekee bali nchi nzima katika Magereza mbalimbali lengo ni kuhakikisha wafanyakazi wa jeshi hilo wanaondokana na adha ya uhaba wa nyumba za kuishi.

Mbali na hilo alisema wamekuwa wakiwafundishwa wafungwa shughuli za ujenzi, kilimo cha kisasa ili wanapotoka baada ya kumaliza adhabu zao wakaendeleze ujuzi waliokuwa nao katika maeneo mbalimbali wanayotoka ikiwemo kuachana na tabia za kihalifu ambazo wamekuwa wakifanya zilizopelekea kupata adhabu ya kifungo.

Katika hatua nyingine amewapongeza wakuu wa gereza la Isanga na Msalato kutokana na usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya Ujenzi katika Magereza hayo.

Alisema wameonyesha jinsi gani wamelipa kipaumbele agizo la Rais kwa sababu hadi sasa baadhi ya nyumba katika Magereza hayo zimefikia hatua nzuri kwenye ujenzi kulingana na muda walioanza kujenga.

“Nawapongeza sana wakuu wa Magereza haya naamini kile kilichokusudiwa katika ujenzi huo kitakamilika,” alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Naye Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma, Keneth Mwambije amemshukuru Kamishna Jenerali kwa kutembelea mradi huo wa ujenzi kuona hatua gani zinaendelea ikiwemo kuwatia moyo wafungwa wanaofanya kazi hiyo.

Alisema wao kama Jeshi la Magereza watahakikisha wanatimiza azma ya serikali ya kutaka jeshi hilo kubuni mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kupitia nguvu kazi walionayo kwa mujibu wa sheria jambo ambalo linaendelea kufanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!