Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Magari ya Serikali yagongana, saba wafariki
Habari Mchanganyiko

Magari ya Serikali yagongana, saba wafariki

Spread the love

WATUMISHI saba wamefariki dunia wakati watatu wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), iliyotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 3 Novemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kuhusu ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Murotto amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea wilayani Kongwa, ni kuegeshwa kwa roli aina ya DAF yenye namba za usajili T161 CBB/T152 CBB, barabarani na kupelekea gari ya ofisi ya CAG aina ya Toyota Land Cruiser (STL 6250) kuigonga kwa nyuma .

Kamanda Murotto ameeleza kuwa, baada ya gari hilo kuligonga roli kwa nyuma, iligongana uso kwa uso na gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser ya PSSSF. Gari ya CAG ilikuwa ianendeshwa na Dickson Kitanda (42) ikitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam, na gari la PSSSF lilikuwa linaendeshwa na Peter Elleson Masamu (35).

Gari la ofisi ya CAG lilikuwa na abiria saba na gari la PSSSF lilikuwa na abiria watatu.

Kamanda Murotto amesema miili ya marehemu imepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Kongwa na majeruhi wamelazwa hos[pitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!