Alvaro Morata

Madrid ‘yaikazia’ Man U kwa Morata

REAL Madrid, mabingwa wa soka nchini Hispania na barani Ulaya, wameendelea kushikilia msimamo wao kutotaka kumuuza mshambuliaji wao Alvero Morata kwa kiasi cha fedha kilicho chini ya Pauni 80 milioni, anaandika Shafiyu A. Kyagulani.

Man United ya England inamuhitaji Morata ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji raia wa Sweeden Zlatan Ibrahimovich ambaye kandarasi yake imefikia ukomo.

Man U ilitenga kiasi cha Pauni 52 milioni, kama dau la kumnasa mhispanmi ahuyo, hata hivyo Madrid wanendelea kukaza kamba wakisema, thamani ya mshambuliaji huyo ni pauni 80 milioni.

Mtendaji mkuu wa Man U, yupo katika mazungumzo na Madrid ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Morata ambaye anaonekana kuhitajika na Kocha mreno Jose Mourinho ili kuiongezea nguvu safu yaye ya ushambuliaji.

REAL Madrid, mabingwa wa soka nchini Hispania na barani Ulaya, wameendelea kushikilia msimamo wao kutotaka kumuuza mshambuliaji wao Alvero Morata kwa kiasi cha fedha kilicho chini ya Pauni 80 milioni, anaandika Shafiyu A. Kyagulani. Man United ya England inamuhitaji Morata ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji raia wa Sweeden Zlatan Ibrahimovich ambaye kandarasi yake imefikia ukomo. Man U ilitenga kiasi cha Pauni 52 milioni, kama dau la kumnasa mhispanmi ahuyo, hata hivyo Madrid wanendelea kukaza kamba wakisema, thamani ya mshambuliaji huyo ni pauni 80 milioni. Mtendaji mkuu wa Man U, yupo katika mazungumzo na Madrid ili kuangalia uwezekano wa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube