Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Madiwani wawashukia maafisa kilimo Chamwino
Habari Mchanganyiko

Madiwani wawashukia maafisa kilimo Chamwino

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

MADIWANI wa Halmashauri ya Chamwino wameitaka idara ya kilimo kuhakikisha inawahisha mbegu bora na pembejeo za kilimo kwa ujumla kwa kuendana na msimu wa kilimo. Anaripoti Dany Tibason, Chamwino … (endelea).

Aidha walisema ucheleweshaji huo kuna hatari ya kupanda mbengu za kienyeji ambazo hazina tija  kwa wakulima na matokeo yake uhalisia wa kilimo unakosa sifa.

Malalamiko hayo yalitolewa mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Athumani Masasi alipokuwa akijibu hoja kwenye mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika Chamwino.

Diwani wa kata ya Mlowa Barabarani, Geogre Malima amesema watumishi wa idara hiyo kazi zao wanazifanya kwa mazoea badala ya kuwahamasisha wakulima kupanda mbegu bora zitakazo kwenda na wakati na msimu wa kilimo.

“Idara yako ya wataalamu wa kilimo wakiwemo maafisa ugani,hawawaendei wakulima kuwahamashisha wakulima juu ya upandaji wa mbegu,hawa wanaweza kusababishia wakakosa mazao ya kutosha maana watapanda mbegu za kienyeji,” alisema.

Naye Peter Chigulu, Diwani wa Igandu aliwataka wataalam hao katika kipindi hili kinachoelekea msimu wa kilimo waache kukaa maofisini bali wawafuate wakulima mashambani.

Alisema kitendo cha kukaa maofisini wakati maeneo yao ni ya mashambani,wanaweza kuisababishia wilaya kuwa na njaa kutokana na wakulima hao kuendelea kulima kilimo kilichopitwa na wakati.

“Tatizo la maafisa wako hao hawaendi na wakati muda mwingi wapo maodisni badala ya kuwafuata wakulima kwa ili kuwahamasisha kilimo cha kisasa na upandaji wa mbegu bora,” alisema Chigulu.

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Buigiri, Keneth Yindi alisema maafisa hao wamekuwa hawawajibiki kwa wakulima ipasavyo kutokana na muda mwingi kuwa maofisini badala ya kuwafikia walengwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Athumani Masasi aliwahakikishi wakulima hao kufikiwa na maafisa Ugani hao ikiwemo na mbegu bora za kisasa.

“Nitahakikisha maafisa hao wa idara ya kilimo wanawajibika ipasavyo kwa wakulima,badala ya kukaa maofisini na sasa ofisi zao zitahamia kwa wakulima huko mashambani,” alisema Masasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!