Baraza la madiwani Manispaa ya Iringa wakiwa kikaoni

Madiwani wa CCM wamsusia Meya kikao

MADIWANI wa CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamegoma kushiriki kikao cha baraza la madiwani kilichotarajiwa kufanyika leo tarehe 7 Novemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkurugenzi wa Mansipaa ya Iringa Mjini ambaye ni Katibu wa kikao hicho, Hamid Njovu ameahirisha kikao hicho hadi tarehe 14 Novemba mwaka huu.

Madiwani wa Chadema ndio waliofika kwa ajili ya kushiriki kikao hicho, lakini idadi ya akidi haikutimia na kupelekea kikao hicho kutofanyika.

Kufuatia mgomo huo, Mwenyekiti wa CCM wilayani Iringa, Said Rubeya amesema madiwani wa CCM wako sahihi kutoshiriki kikao hicho, akisema kuwa meya wa manispaa hiyo, Alex Kimbe (Chadema) alikiuka kanuni.

Rubeya amedai kuwa, katika kikao cha CCM madiwani wa chama hicho walilalamikia ubabe wa meya huyo.

MADIWANI wa CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamegoma kushiriki kikao cha baraza la madiwani kilichotarajiwa kufanyika leo tarehe 7 Novemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Mkurugenzi wa Mansipaa ya Iringa Mjini ambaye ni Katibu wa kikao hicho, Hamid Njovu ameahirisha kikao hicho hadi tarehe 14 Novemba mwaka huu. Madiwani wa Chadema ndio waliofika kwa ajili ya kushiriki kikao hicho, lakini idadi ya akidi haikutimia na kupelekea kikao hicho kutofanyika. Kufuatia mgomo huo, Mwenyekiti wa CCM wilayani Iringa, Said Rubeya amesema madiwani wa CCM wako sahihi kutoshiriki kikao hicho, akisema kuwa meya wa manispaa hiyo, Alex Kimbe (Chadema)…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram