Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madai ya Katiba Mpya, yaibuka upya
Habari za SiasaTangulizi

Madai ya Katiba Mpya, yaibuka upya

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa (THRDC)
Spread the love

ASASI za Kiraia nchini, zimeikumbusha serikali kutimiza ahadi yake ya upatikanaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano, kabla ya mwaka 2021. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo tarehe 28 Septemba 2019, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole-Ngurumwa amesema, suala la Katiba Mpya, ni utekelezaji wa ahadi ya Umoja wa Mataifa (UN).

Amesema, Tanzania ilikubali kufanyia kazi mapendekezo 133 ya haki za binadamu, mbele ya mkutano wa nchi mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UN), jijini Geneva, Uswisi. Mapendekezo hayo yalifanyika mwaka 2016.

“Tanzania ilikuwa miongoni mwa mapendekezo hayo 133 ambayo Tanzania inatakiwa kuyatekeleza katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2016 hadi 2021. Ndani ya mapendekezo hayo, kuna suala la Katiba Mpya,” ameeleza Ngurumwa.

Mratibu huyo alikuwa akitoa taarifa yam waka ya mkutano wa wadau wa asasi za kiraia wa kuthibitisha ripoti ya nusu muhula ya Ripoti ya Mapitio ya Haki za Binadamu (UPR) ya Umoja wa Mataifa, jijini Dar es salaam.

Amesema, pendekezo la upatikanaji wa Katiba Mpya, ni miongoni mwa mapendekezo ya UPR ambayo serikali ya Tanzania haijayafanyia kazi.

Aidha, Ngurumwa amesema asilimia 6 ya mapendekezo hayo yameanza kufanyiwa kazi, ikiwemo ulinzi wa haki za wanawake na watoto, jamii na siasa, uchumi na haki za watetezi wa haki za binadamu.

Amesema, serikali imefanikiwa kukamilisha utekelezaji wa asilimia 7 ya mapendekezo hayo, ikiwemo ulinzi wa haki za watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na mapambano dhidi ya rushwa.

“Asilimia 4 ya mapendekezo ya UPR hayajafanyiwa kazi kabisa na serikali ya Tanzania. Lengo la mkutano huu ni kuikumbusha serikali katika kipindi cha miaka 2 iliyobaki ikamilishe mapendekezo iliyoridhia. Ili 67% ya mapendekezo yaliyotekelezwa nusu yakamilishwe,” ameeleza na kuongeza:

“Mapendekezo yasiyoguswa angalau yaanze kufanyiwa kazi na 12 ya mapendekezo ambayo taarifa zake za utekelezaji hazijulikani, serikali itoe.”

Mkutano huo umeandaliwa na THRDC kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia takribani 90 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Lengo la  Mkutano huo ni kupitia na kuhakiki ripoti hiyo ya UPR ya asasi za kiraia(AZAKI ) ya nusu muhula kabla ya kuiwasilisha katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la UN.

“Asasi za Kiraia Tanzania zinafanya ufuatiliaji wa mapendekezo takribani 133 ya haki za Binadamu kwa kipindi Cha miaka miwili na nusu tangu Tanzania ilipopewa mapendekezo 227 mwaka 2016 na kukubali kufanyia kazi mapendekezo 133 kwa kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2021 na Tanzania itafanyiwa mapitio tena mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,” amesema Ngurumwa.

Amesema, mchakato huo wa UPR umeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Haki za Binadamu, Tume ya haki za Binadamu na utawala Bora( CHRAGG) pamoja na asasi za Kiraia   katika kuhakikisha Tanzania inafanyia kazi mapitio ya mapendekezo yaliyotolewa.

Amesema asasi za Kiraia katika ripoti hiyo ya nusu muhula, zimechanganua  mapendekezo hayo katika makundi manane. Imiwemo haki ya kupata Habari na uhuru wa haki za watoto, haki za watu wenye ulemavu, haki za kijamii na haki za kiuchumi na ardhi.

Makundi mengine ni haki za asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu, haki za kijamii na haki ya kisiasa.

“Ripoti hii pia inaelezea ni kwa kiasi gani Tanzania imeyafanyia kazi mapendekezo hayo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

Aidha ripoti hiyo inalenga kuonyesha hatua ambayo Tanzania imepiga hadi sasa katika kutekeleza mapendekezo hayo pamoja na kuwakumbusha wadau mbalimbali kusaidiana na serikali kuhakikisha mapendekezo hayo yanafanyiwa kazi ipasavyo,” amesema Olengurumwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!