Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Machinga waliamsha ‘dude’ Mwanza
Habari Mchanganyiko

Machinga waliamsha ‘dude’ Mwanza

Polisi akipambana na wamachinga katika jijini Mwanza
Spread the love

WAFANYABIASHARA ndogondogo mkoani Mwanza maarufu kama Machinga, wamepinga hatua ya Mary Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuratibu na kuendesha uchaguzi ‘haramu’ wa viongozi wa wafanyabiashara hao, anaandika Moses Mseti.

Mkuu huyo wa wilaya anadaiwa kuendesha uchaguzi katika ofisi zake, kwa kuwashirikisha machinga 60 pekee huku uchaguzi huo ukiendeshwa wakati muda wa uongozi uliopo madarakani ukiwa hajamalizika.

Said Tembo, mwenyekiti wa machinga, Mkoa wa Mwanza amesema viongozi waliochaguliwa na Tesha hawawatambui na wala hawapo tayari kufanya kazi na watu hao.

“Viongozi hao wamechaguliwa kisiasa kwa lengo la kuminya haki zetu. Waliochaguliwa na DC ni watu ambao katika uchuguzi uliopita walikataliwa na wapiga kura katika kinyang’anyiro hicho kutokana na tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Sh. 10 milioni.

“Hivi ulishaona wapi uchaguzi wa machinga unafanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi halafu baada ya uchaguzi DC (Tesha) anatulazimisha wafanyabiashara tukubali viongozi wake aliowachaguwa?” amesema.

Aman Hussein msemaji wa wamachinga mkoani Mwanza amesema DC Tesha aliendesha uchaguzi bila kuwashirikisha wao kutokana na utaratibu mpya unaotarajiwa kuanza kwa kila machinga na wajasiriamali wote kupewa vitambulisho.

“Kila kitambulisho kimoja cha machinga kitatolewa kwa gharama ya Sh. 6,000/- mkuu wa wilaya na viongozi wake wanataka kupiga dili baada ya kuona viongozi wa sasa hawakubaliani na vitendo hivyo.

Baadhi ya ya viongozi wenzetu wamekamatwa na Polisi baada ya kupinga uchaguzi huo kufanyika kwa amri na usimamizi wa Mkuu wa Wilaya. Binafsi nimepigwa sana na Polisi jamii, mpaka sasa wameniambia nikionekana tena watanikatamata wanipige na kuniachia ulemavu,” amesema.

Viongozi waliokamatwa kwa kupinga uchaguzi huo ni Jamal Mwishehe (mweka hazina), David Dickson (katibu msaidizi) na wengine wawili na mpaka sasa wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Kati (Nyamagana).

Mary Tesha, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, alipotafutwa saa 13:21 mchana, ofisini kwake kuzungumzia suala hilo, alidai kwamba hana muda wa kuzungumza na mwandishi wa habari hizi.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanzaalipotafutwa kuhusu kukamatwa kwa machinga hao, alikiri ni kweli machinga hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kufanya fujo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!