ASASI isiyo ya kiserikali nchini kongo imesema watoto wengi zaidi wanakosa elimu kutokana na mgogoro na mfumo duni wa elimu wa nchi hiyo. anaandika Victoria chance.
Ripoti ya Baraza la Wakimbizi la Norway imebainisha kuwa asilimia 92 ya watoto wenye umri wa miaka sita hadi 11 wamekosa elimu katika miji iliyokumbwa na machafuko ya Kalemie na Tanganyika.
Shule 900 zimebomolewa kutokana na kushamiri kwa machafuko katika mkoa wa Kasai katikati mwa Kongo DRC katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Asasi hiyo imetahadharisha pia kwamba nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika inakabiliwa na hatari ya kupoteza kizazi chake kijacho kwa sababu katika mwaka huu umetolewa mchango wa asilimia nne tu ya fedha za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya sekta ya elimu ya Kongo DRC.
Baraza la Wakimbizi la Naorway limeongeza kuwa watoto waliotimiza umri wa kwenda shule wanachangia zaidi ya asilimia 17 ya watu wapatao milioni 3.8 waliopoteza makaazi yao nchini humo katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Leave a comment