Mabasi ya Mwendokasi

Mabasi 165 ya mwendokasi kuongezwa Dar

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema mchakato unafanyika kununua mabasi 165 ili kupunguza adha ya usafiri wa mradi wa mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 13 Mei 2020 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati akijibu swali la Aysharose Mattembe, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aysharose amesema uamuzi wa Serikali kutengeneza miundombinu ya usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi ulilenga kuondoa kero kwa wananchi jijini Dar es Salaam, lakini usafiri huu umekuwa kero kubwa kwa watumiaji ikiwemo kujaza abiria bila kujari athari za watumiaji.

“Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti ujazaji abiria pamoja na kuweka utaratibu mzuri kwa watumiaji wake,” ameuliza

Akijibu swali hilo, Waziri wa Tamisemi amesema, ili kupunguza msongamano wa abiria, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (DART) unaendelea na taratibu za ununuzi ili kumpata mzabuni atakayeongeza idadi ya mabasi kutoka 140 yaliyopo sasa hadi 305.

About Masalu Erasto

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!