Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Maandamano yamng’oa Rais wa Mali
KimataifaTangulizi

Maandamano yamng’oa Rais wa Mali

Spread the love

RAIS wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kujiuzulu pamoja na Waziri Mkuu wake, Boubou Cissé muda mfupi baada ya wanajeshi waasi kuwakamata na kuwaweka kizuizini katika kambi ya jeshi mji mkuu wa Bamako. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Keita ametangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatano tarehe 19 Agosti 2020 kupitia televisheni ya taifa akisema anavunja Serikali na Bunge.

“Natangaza kujiuzulu kuanzaia sasa. Sitaki damu imwagike ili mimi kuendelea kubaki madarakani,” amesema Keita.

Keita na waziri mkuu wake walikamwatwa na jeshi baada ya maandamano yaliyodumu kwa miezi kadhaa kumtaka Rais huyo kung’atuka madarakani akishutumiwa kusababisha hali mbaya ya uchumi.

Pia, kiongozi huyo wa Mali alikuwa akishtumiwa kushindwa kuzuia makundi ya wapiganaji wa Kiislamu ambayo yamesasbabisha kutokuwapo kwa amani ya nchi hiyo.

Baada ya jeshi hilo kuwatia kizuizini, Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, Umoja wa Mataifa, Ufaransa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zililaani uasi huo na kuonya jaribio lolote la kubadili madaraka kinyume na katiba katika taifa hilo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alilitaka jeshi hilo “kuachiwa haraka na bila masharti” kwa Keita na Cisse.

ECOWAS kwenye taarifa yake, iliwataka wanajeshi kurejea kambini na kujizuia dhidi ya “kitendo chochote kinyume na katiba” na kujaribu kutatua tofauti za kisiasa kupitia mazungumzo.

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya ulisema “unalaani jaribio la mapinduzi nchini Mali na unakataa mabadiliko yasiyo ya kikatiba” huku taarifa hiyo ikisema hatua hiyo haiwezi kuwa suluhisho la mgogoro mkubwa wa kisiasa ambao umeikumba Mali kwa miezi kadhaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!