Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Wamepanga kunikamata 
Habari za Siasa

Maalim Seif: Wamepanga kunikamata 

Maalim Seif Shariff Hamad
Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, mwanachama namba moja wa Chama cha ACT-Wazalendo amedai kwamba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jeshi la Polisi wamepanga kumkamata kabla ya Uchaguzi Mkuu 2020. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

 Maalim Seif alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akihutubia wanachama wapya wa tawi jipya la ACT-Wazalendo la Mtendeni mjini Zanzibar.

Maalim Seif amedai, viongozi wa CCM, wamepanga wamkamate kwa kisingizio kuwa, amekuwa akifanya uchochezi kupitia kauli zake za hivi karibuni ikiwemo ya kutetea haki ya Wazanzibari kwenye muungano.

Amesema, amepata taarifa kuwa mpango wa kumkamata unatarajiwa kutekelezwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao, kwa lengo la kumzuia kugombea urais wa Zanzibar.

“Najua wamekutana na kupanga kunikamata, lengo lao kubwa likiwa ni kunizuia kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2020. Kwani mtu hawezi kuchaguliwa akiwa jela,” amehoji Maalim Seif na kuongeza:

“Iwapo nitaamua kugombea, na chama changu kikaniteua, hakuna cha kunizuia hata nikiwa na kesi. Na mimi nawaambia CCM, wamsimamishe mtu yeyote, nitamshinda tu.”

Akizungumza na wakazi wa Mtendeni kwenye uzinduzi wa tawi hilo, Maalim Seif amesema anachobaini sasa kwenye siasa za Zanzibar, ni kuwepo mkakati wa kumuandama yeye na sio chama anachohamia.

 “Mimi nilidhani tukiwaachia chama, wataacha kumfuatafuata Seif Shariff… tumewaachia chama cha CUF lakini bado wanaendelea kunifata hukuhuku ACT. Kumbe ugomvi wao ni Seif. Basi nawaambia hawa watu kuwa, mtapata taabu sana kwa kuniandama mimi Seif Shariff,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif ambaye alikuwa katika Chama cha Wananchi (CUF), alihama chama hicho tarehe 18 Machi 2019 na kujiunga na ACT-Wazalendo, muda mfupi baada ya Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kumthibitisha Prof. Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.

Prof. Lipumba alijiuzulu kwa hiari yake tarehe 5 Agosti 2015, akieleza kuwa hawezi kuendelea kuongoza chama hicho kutokana na tofauti na wenzake hivyo hawezi kusaliti nafsi yake kubakia mamlakani.

Siku hiyo aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, atabakia mwanachama muaminifu na kujitolea kutoa ushauri kwa chama hicho alichojiunga wakati taifa likijiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. CUF ilimteua yeye kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini miezi 10 baada ya kuwa nje ya wadhifa huo, alijitokeza na kutangaza kuwa, ametengua uamuzi wa kujiuzulu na amerudi kwenye wadhifa uleule na kwamba, alikuwa anasubiri maelekezo ya Katibu Mkuu wa chama ili aanze rasmi kazi zake.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!