Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Uvumilivu wetu umefika mwisho
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif: Uvumilivu wetu umefika mwisho

Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF.
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amesema viongozi na wanachama wa chama hicho wapo tayari kwa lolote kutokana na uhujuma wanazofanyiwa na serikali, anaandika Shabani Matutu.

Maalim Seif amebainisha kuwa hajashindwa kazi, kama vibaraka wa serikali wanavyosema bali anaendelea kufanya kazi za chama hicho na muda si mrefu ataanza rasmi ziara yake jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake Zanzibar.

Maalim Seif amewambia wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuwa sema kuwa amekuwa na ziara ya kuimarisha chama chicho katika kisiwa cha Unguja, hata hivyo ameamua kukatisha ili kuzungumza na Watanzania kutokana hali ya kisiasa iliyopo.

“Nataka ifahamike kuwa mgogoro wa kupandikizwa kwa kumtumia Profesa Ibrahim Lipumba hauna lengo la kuiua CUF bali upinzani na hasa Ukawa, ambapo lengo pana ni kuua demokrasia Tanzania kwa kuhujumu na kuzuia taasisi zote zinazooneka kuwa ni nguzo imara za demokrasia yetu,” amesema.
Amesema kuwa kuna mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kuua demokrasia kwa kunyamazisha taasisi zinazothubutu kutoa mawazo tofauti na yale ya watawala walioingia madarakani mwaka 2015.

Maalim Seif amesema kuwa kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima. Kuzuiwa kwa matangazo mubashara ya mikutano ya Bunge ni miongoni mwa mbinu za uminyaji wa demokrasia hapa nchini.

Pia ameeleza juu ya kufinywa kwa bajeti ya shughuli za Bunge na hasa Kamati za Bunge ili zisiweze kufanya kazi ya kuisimamia serikali, kuchunguza mapungufu ya viongozi na watendaji wa serikali.

“Wanawakamata, kuwabughudhi, kuwalaza ndani na kuwafungulia mashtaka wabunge wa upinzani hasa wale wanaoonekana kuwa mwiba mkali kwa watalawa ili kuwatisha na kuwanyamazisha wasifanye kazi yao ya kuwakosoa watawala,” amesema.

Maalim amesema ghiliba za utawala uliopo madarakani zimefika mpaka katika mhimili wa mahakama ambapo serikali inatoa maagizo hadharani ya jinsi ya kuamua kesi na hata kuahidi kuwapa fedha wanazozihitaji kwa ajili ya uendeshaji wa mahakama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!