Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Sina wasiwasi na mapingamizi
Habari za Siasa

Maalim Seif: Sina wasiwasi na mapingamizi

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, hana wasiwasi juu ya mapingamizi aliyowekea Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ili asipitishwe kugombea nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 siku moja baada ya vyama vya DP na Demokrasia Makini kumuwekea mapingamizi ZEC.

Kwa mujibu wa Thabiti Faina, Mkurugenzi wa Uchaguzi ZEC, alisema Maalim Seif hakuteuliwa kutokana na mapingamizi hayo, ambayo yalitokana na dosari katika ujazaji wa fomu zake.

Akizungumzia sababu hizo, Maalim Seif amesema, yeye ana uhakika hajafanya kosa lolote katika ujazaji wa fomu zake, hivyo anasubiria maamuzi ya NEC, huku akisisitiza ana amini tume hiyo itatenda haki.

Dk. Hussein Mwinyi, mgombe wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM akichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo

“Tumekubaliana kila upande kutoa hoja zake halafu tume itaamua, mimi sina wasiwasi kwa sababu na hakika sijafanya kosa lolote , iko timamu. Lakini hawajui mapungufu yao wananiimarisha zaidi kuliko wakati wowote,” amesema Maalim Seif.

Wakati Maalim Seif akishindwa kuteuliwa, ZEC iliwateua wagombea 16 kuwania nafasi hiyo ya juu kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye anamaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa Katiba.

Wagombea hao 16 ni; Hussein Juma Salim (TLP), Issa Mohamed Zonga (SAU), Said Soud Said (AAFP), Said Issa Mohamed (Chadema), Khamis Fakhi Mgau (NRA) na Mfaume Hamis Hasaan (NLD).

Wengine ni; Dk. Hussein Mwinyi (CCM), Hamad Mohamed (UPDP), Shafii Hassan Suleiman (DP), Othuman Rashid Khamis (CCK), Ameir Hassan Ameir (Demokrasia Makini), Ali Omar Juma (Chaumma), Hamad Rashid (ADC), Juma Ali Khatib (Ada Thadea), Mussa Haji Kombo (CUF) na Mohamed Omar Shaame wa UMD.

Licha ya mgombea huyo Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo kuwekewa mapingamizi, pia wagombea wake wa ubunge katika majimbo yote visiwani humo wamewekewa mapingamizi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 na Salim Bimani, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, wanasheria wa chama hicho wako katika taratibu za kujibu mapingamizi hayo.

Aidha, Bimani alisema wagombea uwakilishi katika majimbo 37 wamewekewa pingamizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!