Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Nani atanitongoza?
Habari za Siasa

Maalim Seif: Nani atanitongoza?

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameeleza kwamba msimamo wake katika siasa unamweka mbali na ‘wanaotongoza’ wanasiasa ili kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akijibu swali la mwandishi wa habari wa Kampuni ya Habari ya Mwananchi Communication, leo tarehe 4 Machi 2020 wakati wa mahojiano yake, Maalim Seif amesema CCM wasidhani kama anaweza kuhamia chama hicho kwa kuwa si mwanasiasa malaya.

“Mwalimu Nyerere alisema kuna wanasiasa malaya, kwanza nani atanionoza mimi?…kwa sababu wanajua msimamo wangi,” amesema Maalim Seif na kuongeza:

“Mini binafsi siasa ni my second wife (mke wangu wa pili), haikuwa chaguo langu kuingia kwenye siasa, nilitumbukizwa kwenye siasa.”

Mkongwe huyo wa siasa za upinzani visiwani Zanzibar amesema, uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, CCM itaanguka zaidi ya ilivyoanguka miaka yote visiwani Zanzibar.

Alipoulizwa amejipangaje kutokana na malalamiko yake ya mara kwa mara ya kupokwa ushindi, Maalim Seif amesema uchaguzi huu katu hawawezi kuchaguliwa rais na mamlaka zilizopo madarakani bali wananchi wa Zanzibar.

“Uchaguzi wa 2020, mwaka huu CCM tunaishinda vibaya sana, pili tukishinda tutalinda ushindi wetu, hatukubali tena deep state ituchagulie viongozi …,” amesema na kusisitiza:

“This time (kipindi hiki) nasema tena, hatutakubali deep state kutuwekea marais, rais atatokana na matakwa ya wananchi, na tuko tayari. Waliyofanya yote huko nyuma lakini hivi sasa ndio basi. Watwala wajue ths time hatutakubali kabisa.”

Amesema, kuna mikakati mbalimbali inaendelea kufanywa na CCM katika kurubuni, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), kujinunga na CCM kwa kuwapa vitisho endapo watagoma

“Kuna other forces (nguvu nyingine) watu kwenda CCM, miaka yote hawapati chochote Pemba, na hii inawauma sana. Pemba wanajitambua.

“Habari ambazo tunazo, mikakati inapangwa ili kuwanunua wagombea wa ACT (ACT-Wazalendo) Pemba, na kama watakuwa shupavu hawakubali, wanatekwa.”

Akizungumzia kukutana na Rais John Magufuli jana tarehe 4 Machi 2020, Maalim Seif amesema, hatua ile ni ya kwanza na baada ya hapo mambo mengine yatafuata.

Alipoulizwa ahadi ya Uchaguzi Huru na haki inayotolewa na Rais Magufuli kama itatekelezwa kwa asilimia 100?  amesema hatarajii hilo.

“Hayo madaraka hayapo kwangu, yapo kwa rais. Siwezi kuwambia kwamba nima matarajio kwa asilima 100 kwamba yatafanyika. Ushauri ni kwamba wakati umefika, hata kama muda ni mfupi lakini it can be done (yanaweza kufanyika).

“Sisi Zanzibar hatukuwa na muda (maridhiano), ila kulikuna na nia njema. Suala kubwa ni Katiba, kama kungekua na nia njema pande zote, tayari kuna mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba sio yale ya CCM, tuangalie yale mapendekezo yanasema nini, yakaangaliwe hayo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!