Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif akabidhiwa cheo ACT-Wazalendo, yumo Jussa, Bimani, Mazrui
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif akabidhiwa cheo ACT-Wazalendo, yumo Jussa, Bimani, Mazrui

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimemteua Maalim Seiff Sharif Hamad, kuwa mshauri mkuu wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Gwiji huyo wa siasa za upinzani nchini, aliyejiunga na chama hicho mwanazoni mwa mwaka huu na kupewa kadi No. 1, atakuwa ndiye mshauri wa masuala ya kisasa na uimarishaji wa chama hicho, cheo ambacho amekabidhiwa kuanzia jana tarehe 9 Juni 2019.

Kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo, Maalim Seif alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye alihama chama hicho kutokana na mgogoro wa muda mrefu kati yake na Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho Taifa.

Uamuzi wa Maalim Seif kuhama CUF ulitekelezwa tarehe 18 Machi 2019 baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Chanzo cha mgogoro huo ni pale Prof. Lipumba, alipotaka kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti licha ya kuandika barua ya kujiuzulu kwa hiyari yake mwaka 2015 muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo akizungumza na MwanaHALISI Online amesema kuwa, kamati  kuu ya chama hicho iliyoketi tarehe 9 Juni 2019, kwenye ofisi zao ndogo Magomeni, jijini Dar es Salaam ilifikia uamuzi huo ikiwa ni pamoja na kujaza nafasi zingine zilizoachwa wazi.

Ado ameeleza kuwa, Maalim Seif ameteuliwa kwenye nafasi hiyo kuziba nafasi aliyoacha Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alitimka Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kumteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Ado amesema kuwa, pia wameteuliwa wajumbe wengine wa Kamati Kuu ambao ni Theopista Kumwenda, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ndani ya chama hicho; Mwajabu Dhahabu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii.

Wengine ni Fatma Fereji, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Eddy Riyami ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano na Timu ya Ushindi (CUF).

kamati hiyo imechagua wenyeviti wa kamati mbalimbali ambapo Nassor Mazrui, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi. Kabla ya hapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu (CUF)-Zanzibar.

Salim Bimani ameteuliwa kuwa Mwenyekitii wa Kamati ya Itikadi, Masiliano na Uenezi, kabla ya hapo alikuwa Katibu Mwenezi CUF.  Jorani Bashange ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi, awali alikuwa Mkurugenzi wa Fedha CUF.

Muhonga Ruhwanya ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Organizesheni na Mafunzo na Wanachama huku Isamil Jussa akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji ambayo ni kamati mpya ndani ya chama hicho. Awali Jussa alikua Mkurugenzi wa mambo ya nje ya CUF.

Ado ameeleza kuwa, kamati hiyo imemteua Shaweji Mketo kuwa Katibu wa Kamati ya Organizasheni, Mafunzo na Wanachama. Awali Mketo alikuwa aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF.

Kulthum Mchuchuli ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Katiba na Sheria, awali alikuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria CUF.

Mbarala Maharagande ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Uadilifu ambapo awali alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF. Rachiel Kimambo ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Mikakati,Usimamizi na Ufuatiliaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!