Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: CCM ijiandae kuondoka itake isitake
Habari za Siasa

Maalim Seif: CCM ijiandae kuondoka itake isitake

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, chama hicho kimejiandaa kushika dola na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijiandae kuondoka ‘taka isitake’ baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea)

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 1 Septemba 2020 katika mkutano wa uzinduzi wa kampini za urais katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mpilipili.

Bernard Kamilius Membe ndiye mgombea urais na Profesa Omar Fakih Hamad, mgombea mwenza.

Akizindua kampeni hizo, Maalim Seif  amesema, msimamo wa chama hicho sasa ni kukataa kuonewa.

Amesema wagombea wa ACT-Wazalendo wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Bernard Membe-ACT-Wazalendo

“Chama cha ACT-Wazalendo sasa kimekuwa ni tishio kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  ndio maana wagombea wetu wameenguliwa, msimamo wetu sasa maonevu basi,” amesema Maalim Seif ambaye ni mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho.

“Sasa huu ni wakati wa kuikomboa nchi yetu na mkombozi ni ACT-Wazalendo, tunahitaji serikali itakayoleta maendeleo kwa wananchi, itakayoleta uhuru kwa wananchi na Serikali hiyo itaongozwa na Bernard Kamilius Membe,” amesema Maalim Seif huku akishangiliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!