Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif awekewa pingamizi, 16 wateuliwa
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif awekewa pingamizi, 16 wateuliwa

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeshindwa kumteua Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT-Wazalendo baada ya kuwekewa pingamizi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja … (endelea).

Leo Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020, ZEC imewateua 16 kati ya 17 waliochukua fomu na kurudisha kugombea urais wa visiwa hivyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Thabiti Faina amesema, Maalim Seif ameshindwa kuteuliwa kutokana na vyama viwili vya DP na Demokrasia Makini kumwekea pingamizi.

Amesema, mapingamizi ya vyama hivyo yanafanana ambayo yanahusu ujazwaji wa fomu za Maalim Seif kutokuwa sahihi.

Mkurugenzi huyo amesema, baada ya Maalim Seif kujibu mapingamizi hayo, tume hiyo itaamua kama ni kumteua au la.

Benard Membe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe pamoja na Maalim Seif

Maalim Seif ndiye mgombea pekee anayewamia kugombea nafasi hiyo mara sita kati ya wote 17 waliojitosa kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye ananaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba.

Alianza kugombea mwaka 1995, 2000,2005,2010 na 2015 kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na sasa anapambana kugombea mara ya sita kupitia ACT-Wazalendo.

Jumanne ya tarehe 8 Septemba 2020, Maalim Seif akizungumza katika Kongamano la Vijana la ACT-Wazalendo visiwani Zanzibar aligusia taarifa za kuwekewa mapingamizi.

Aliwaeleza vijana hao kuna watu wa vyama vingine wamepanga kumwekea mapingamizi ili asiteuliwe kugombea huku akiwakaribisha kufanya hivyo.

“Nasikia kuna watu washapangwa na vyama vingine kuniwekea pingamizi, nawakaribisha, sababu kuniwekea pingamizi yeye anakuja kutoa haja zake na ushahidi wake na mimi naujua vilevile.”

“Sioni kama kuna pingamizi yoyote kama itasimama juu yangu. Mimi nimezaliwa Mtambwe hamjui ninyi? Ndiyo sifa ya kwanza ya mgombea urais awe Mzanzibar wa kuzaliwa sio Mzanzibar mkaribishi,” alisema Maalim Seif.

Wagombea 16 walioteuliwa na ZEC ambao kesho Ijumaa wanaweza kuanza kampeni ni; Hussein Juma Salim (TLP), Issa Mohamed Zonga (SAU), Said Soud Said (AAFP), Said Issa Mohamed (Chadema), Khamis Fakhi Mgau (NRA) na Mfaume Hamis Hasaan (NLD).

Wengine ni; Dk. Hussein Mwinyi (CCM), Hamad Mohamed (UPDP), Shafii Hassan Suleiman (DP), Othuman Rashid Khamis (CCK), Ameir Hassan Ameir (Demokrasia Makini), Ali Omar Juma (Chaumma), Hamad Rashid (ADC), Juma Ali Khatib (Ada Thadea), Mussa Haji Kombo (CUF) na Mohamed Omar Shaame wa UMD.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!