Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Maalim Seif atoa sharti kukubali kushindwa Z’bar

Spread the love

MGOMBEA urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema, ili akubali kushindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, lazima uchaguzi huo uwe huru na haki. Anaripoti Mwandishi Wetu, …(endelea).

Akizungumza na kituo cha habari cha Uingereza (BBC), jana Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020, Maalim Seif amesema, ikiwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki, atampongeza mshindani wake Dk. Hussein Ali Mwinyi, mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, sina tatizo, nitampongeza Dk. Hussein Mwinyi,” amesema Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho Taifa.

Nguli huyo wa siasa za upinzani Zanzibar, tayari amewaweka wafuasi wa chama chake tayari kwa ajili ya kile alichosema ‘kutetea haki yao,’ iwapo itapokwa baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi huo mkuu.

Tarehe 20 Oktoba 2020, Maalim Seif alipozunguma na waandishi wa habari alisema, tofauti na chaguzi zilizopita, uchaguzi wa safari hii hatomzuia mtu yeyote kujitokeza na kutetea haki yake.

“Siku zote tulikuwa tukitahadharisha kwa kudhani kwamba wenzetu ni waungwana. Kwamba wenzetu watatilia maanani tunayozungumza, na siku zote mimi niseme, nilikuwa nawazuia watu wasiingie barabarani, nyote mnajua.

“Mwaka huu simzuii mtu, atakayeamua kufanya lolote kutetea haki yake, simzuii. Kwa hiyo, ngojeni muziki tarehe 27 na 28 mtauona,” amesema Maalim Seif.

“Tuiache demokrasia ifuate mkondo wake kwa amani. Tumekishwavumilia vya kutosha, sasa tunakwenda tarehe 27 na tarehe 28 tukiwa tayari kwa lolote lile litakalotokea. Kulinda demokrasia na kulinda haki ya Wazanzibari kumchagua rais wanayemtaka.”

Alisema, katika uchagzi wa mwaka huu, Wazanzibari hawawezi kuvumilia haki yao kuporwa na kwamba, tayari wameishapitia mengi katika maisha yao.

“Nataka kutahadharisha kuwa Wazanzibari wamedhamiria kulinda demokrasia kwa gharama yoyote, katu hatukubali kuendelea kudharauliwa. Wazanibari wameishapitia mengi, wamevuta subira na uvumilivu mkubwa na kupigiwa mfano. sasa imetosha.

MGOMBEA urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema, ili akubali kushindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, lazima uchaguzi huo uwe huru na haki. Anaripoti Mwandishi Wetu, …(endelea). Akizungumza na kituo cha habari cha Uingereza (BBC), jana Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020, Maalim Seif amesema, ikiwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki, atampongeza mshindani wake Dk. Hussein Ali Mwinyi, mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, sina tatizo, nitampongeza Dk. Hussein Mwinyi,” amesema Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho Taifa. Nguli huyo wa siasa za…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!