Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif ataja hasimu wake Uchaguzi Mkuu 2020
Habari za Siasa

Maalim Seif ataja hasimu wake Uchaguzi Mkuu 2020

Spread the love

HASIMU wangu na wetu sisi Chama cha ACT-Wazalendo kwenye siasa si Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wala Chama cha NCCR-Mageuzi pia vyama vingine vya upinzani, lah! Anaripoti Faki Sosi, Mtwara … (endelea).

Hasimu wetu mkubwa ndio hasimu wenu nyinyi wakazi wa Mtwana na Tanzania yote, naye ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutunyima fursa zilizo halali kwentu.

Kiongozi huyo nguli visiwani Zanzibar ametoa kauli hiyo tarehe 21 Julai 2020, alipokuwa wilayani Tunduru kwenye ziara ya viongozi wa chama hicho.

“Lazima tudumishe umoja. Malengo yetu ni mamoja, vita vetu ni vimoja, Chadema si adui, NCCR ni muathirika kama wewe, usipoteze muda kupambana na Chadema au NCCR, pambana na hili dude, tusipingane sisi wenyewe kwa wenyewe, tupambane na CCM tutaiangusha.”

https://www.youtube.com/watch?v=78UhroavGdk

Amesema, vyama vya upinzani vipo kwenye mazungumzo ya kujenga umoja ili kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

“Nitoe siri mchakato wa kutafuta umoja umeamza, yaliyopita si ndolwe. Tutachukua tahadhari zote,” amesema.

Pia amesema, siri ya ushindi wa uchaguzi ni kufanya kazi ya kisiasa kwa bidii na kuhakikisha wagombea wote wamejaza fomu vizuri na kuzirejesha kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!