July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif ashangaa viongozi kubeza tukio la Mbowe

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif  Sharif Hamad ameliita tukio la kushambuliwa kwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni “kitendo kibaya kabisa, kitendo cha kishezi kabisa.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Maalim Seif  ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa ikiwamo tukio hilo na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akitoa taarifa ya awali ya tukio hilo alisema, Mbowe alishambuliwa na watu watatu kwa kumkanyanga kanyanga na kumvunja mguu wa kulia.

Mbowe alifikwa na tukio hilo usiku wa kumkia jana Jumanne wakati akipanda ngazi za kuingia nyumbani kwake Area D jijini Dodoma. Kwa sasa Mbowe amelazwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam

Katika mazungumzo yake, Maalim Seif amesema, “baadhi ya viongozi kama vile wanafurahia, wanakejeri, najiauliza hivi jamani Tanzania tumepoteza ubinadamu kiasi gani?”

“Mwenzako anafikwa na maafa, badala ya kumuhurumia wewe una mkejeri,” amehoji Maalim Seif aliyewahi kuwa Makamu Kwanza wa Rais Zanzibar

error: Content is protected !!