Maalim Seif apigwa ‘stop’ Clouds TV

Spread the love

MAMLAKA katika kituo cha televisheni cha Clouds, jijini Dar es Salaam, imeagiza kufutwa kwa mahojiano kati ya kituo hicho na mwanasiasa mkongwe Visiwani Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mahojiano kati ya Maalim Seif na kituo hicho, yalipangwa kufanyika leo, tarehe 28 Machi na kurushwa moja kwa moja (live), kupitia kipindi kilichopewa jina la Clouds 360.

Kwa mujibu wa Ado Shaibu, katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha ACT-Wazalendo, televisheni ya Clouds ndiyo iliyoomba kuwapo mahojiano hayo na Maalim Seif.

Anasema, “Clouds TV imefuta ratiba ya mahojiano hayo kwa kile walichoeleza, sababu zilizo nje ya uwezo wao.”

Maalim Seif ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Alijiunga na ACT- Wazalendo na kukabidhiwa kadi ya heshima ya mwanachama Na. 1, mapema wiki iliyopita, kufuatia Mahakama Kuu, kumtangaza Prof. Ibrahim Lipumba, kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

MAMLAKA katika kituo cha televisheni cha Clouds, jijini Dar es Salaam, imeagiza kufutwa kwa mahojiano kati ya kituo hicho na mwanasiasa mkongwe Visiwani Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Mahojiano kati ya Maalim Seif na kituo hicho, yalipangwa kufanyika leo, tarehe 28 Machi na kurushwa moja kwa moja (live), kupitia kipindi kilichopewa jina la Clouds 360. Kwa mujibu wa Ado Shaibu, katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha ACT-Wazalendo, televisheni ya Clouds ndiyo iliyoomba kuwapo mahojiano hayo na Maalim Seif. Anasema, “Clouds TV imefuta ratiba ya mahojiano hayo kwa kile walichoeleza, sababu zilizo nje ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!