January 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif akubali yaishe, akumbusha machungu ya uchaguzi 

Spread the love

HATIMAYE Maalim Seif Hamad, mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, amekubali yaishe. Ameapishwa kuwa Makamo wa Rais wa Kwanza, katika serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUKI). Anaripoti Regina Mkondo, Dar es Salaam … (endelea).

Katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kuapishwa leo, tarehe 8 Desemba, Ikulu ya Zanzibar, Maalim Seif alisema, uamuzi wake na chama chake, kuridhia kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa, umetokana na kile alichoita, “dhamira njema ya kuzika tofauti zao za kisiasa.”

         Soma zaidi:-

Alisema, wamekubali kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ili wapate fursa ya kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, unaodaiwa kugubikwa na vitendo vya uvujinfu wa amani na hivyo kuacha majeraha makubwa kwa baadhi ya wananchi na vyama vya siasa.

Amesema, maamuzi yao ya kuridhia kuingia serikalini, yamelenga kurejesha umoja wa kitaifa na kuzika tofauti hizo, ili kuirejesha Zanzibar katika amani na mshikamano.

Amesema, “ni imani yangu binafsi na chama changu, kwamba wajibu wa mwanzo wa serikali hii, itakua ni kuunganisha wananchi, iki kuweza kuwa na amani. Kwa muktadha huo, nimekubali kushirikiana na serikali hii, ili kuhakikisha yaliyitokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi hayajirudii tena.”

Amesema, yeye na wenzake wamekubaliana kuingia kwenye serikali, ili kuwaunganisha Waazanzibar na kuongeza, “…uchaguzi mkuu uliyopita, umepita na changamoto nyingi ambazo zimetufunua macho, kuwa na majibu ya kisheria na katiba pekee hautoshi kutufikisha katika matamanio yetu ya maridhiano.”

Maalim Seif amesema, “tunayo haja kutafuta majibu na muafaka wa kitaifa.”

Mwenyekiti huyo wa ACT-Wazalendo ambaye amepata kushika nafasi hiyo wakati wa utawala wa Dk. Mohammed Alli Shein amesema, “Zanzibar imegewanyika na haiwezi kupiga hatua yoyote ya maendeleo, bila kuwapo mshikamano.”

Ameongeza, “amani na utulivu ndio majibu ya kuivusha Zanzibar kutoka ilipo sasa kwenda kwenye Zanzibar iliyopiga hatua katika mendeleo. Kwa sababu ya muelekeo huo, ndio maana ACT na mimi nimeridhika kushirikiana na CCM kujenga Zanzibar mpya.”

Amewaomba viongozi wa Serikali hiyo kutumia nyadhifa zao kutibu majeraha ya wahanga wa uchaguzi.

“Viongozi tutibu majeraha ya waathirika kwa kuonesha kwa vitendo. Tunayo nia ya dhati na maridhiano ili tujenge Zanzibar moja yenye kuheshimu haki na kujenga umoja,” ameeleza.

Maalim Seif amesema, yeye binafsi ameahidi kutoa ushirikiano kwa Dk. Mwinyi, mawaziri na watumishi wengine wa umma katika kuwatumikia wananchi wa Zanzibar.

Amesema, “Rais Dk. Hussen Mwinyi, nitakupa ushirikiano, nitawapa ushirikiano mawaziri wote, wakuu wa mikoa wote na wengine waote, watakaohitaji.  Nitawapa hata ushauri wangu kwa yoyote atakayehitaji ushauri wangu, roho yangu mimi iko wazi.”

Amewaomba Wazanzibar wote kusahau machungu ya uchaguzi huo, kisha wakubali maridhiano yaliyoafikiwa baina ya chama chake na Serikali ya Zanzibar iliyochini ya CCM.

Amesema, “Wazanzibar wote walioko ndani na nje, wakubali kunyoosha na kupokea mkono wa mardhiano tumeze machungu ya uchaguzi. Ni wakati wa kuzika historia hii na kuijenga Zanzibar.

“Maridhiano yanafungua milango ya kuwezesha  Serikali kujenga upya pale palipovunjwa, vurugwa na kuharibika. Bila ya hatua hii, mageuzi tunayotaka hayawezi kufanyika na kusimamia ipasavyo kwa kiwango kinachokidhi matakwa ya wananchi.”

Uamuzi wa ACT-Wazalendo kushiriki katika SUK ulipingwa na baadhi ya watu wakisema kwamba umewasaliti Wazanzibar walioathirika na uchaguzi huo.

Hata hivyo, Maalim amewajibu akisema kwamba kususa kushiriki katika SUKI hakutatibu majeraha ya uchaguzi.

Akifafanua hilo, Maalim Seif amesema, “katika kuwasaidia wale wenye imani na wenye ufahamu potofu juu ya SUKI napenda kutumia mfano wa rahisi, SUKI ni sawa na chombo cha usafiri kwa msafiri yeyote awe baharini au angani, lengo lake sio kuingia katika meli, ndege au gari; lengo lake kufika safari aliyoipanga.

“Safari ya Wazanzibar ni maridhiano ya kweli, mshikamano na umoja wa kitaifa. Kufika kwa wakati kwa serikali ya SUKI ni wajibu wetu sote ambao tumepewa jukumu la kuiongoza Serikali kuhakikisha tunafanikisha chombo hiki kinafika katika safari hii.”

Maalim Seif alipendekezwa na ACT-Wazalendo kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kisha mapendekezo hayo kuthibitishwa na Rais Dk. Mwinyi, baada ya chama chake  kushika nafasi ya pili katika kura za uchaguzi wa urais wa Zanzibar.

Awali, ACT-Wazalendo kilisuasua kufanya uteuzi huo sambamba na kushiriki katika SUK, wakipinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

error: Content is protected !!