Maalim Seif, M/kiti ACT-Wazalendo Taifa

Maalim Seif akamatwa Z’bar 

Spread the love

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad inadaiwa amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha kupigia kura cha Garagara visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Maalim Seif amekutwa na kadhia hiyo leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020 ikiwa ni siku ya kwanza ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu visiwani huo utakaohitimishwa kesho Jumatano.

“Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Maali Seif Sharif Hamad amekamatwa muda huu na vyombo vya dola wakati akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Garagara. Taarifa zaidi zitawajia,” inaeleza taarifa ya ACT-Wazalendo.

Taarifa ya chama hicho inasema, Maalim Seif amepelekwa Kituo cha Polisi Ziwani kwa mahojiano.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar inaruhusu watumishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na watumishi wengine watakaosimamia Uchaguzi Mkuu wa kesho Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kupiga kura siku moja kabla ya uchaguzi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari mbalimbali ikiwemo kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu suala hili.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad inadaiwa amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha kupigia kura cha Garagara visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar ... (endelea). Maalim Seif amekutwa na kadhia hiyo leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020 ikiwa ni siku ya kwanza ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu visiwani huo utakaohitimishwa kesho Jumatano. "Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Maali Seif Sharif Hamad amekamatwa muda huu na vyombo vya dola wakati akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Garagara. Taarifa zaidi zitawajia," inaeleza taarifa ya ACT-Wazalendo. Taarifa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

One comment

  1. jamani simba kwanini mtanyima raha ni mzimu gani huo unaovuruga timu yetu?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!