Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif ahofia ‘kukatwa’ urais Z’bar
Habari za Siasa

Maalim Seif ahofia ‘kukatwa’ urais Z’bar

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mgombea urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ameonesha wasiwasi wa kukwamishwa katika kinyang’anyiro hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Akizungumza katika Kongamano la Vijana wa ACT-Wazalendo tarehe 8 Septemba 2020 visiwani humo, Maalim Seif amedai, kuna baadhi ya watu wa vyama vingine wamepanga kumuwekea pingamizi katika Tume ya Uchaguzi (ZEC), ili asiteuliwe kugombea.

Amesema, anawakaribisha watu wanaotaka kumuwekea pingamizi akisema, kwamba anafahamu namna ya kupangua pingamizi zao.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akimkabidhi fomu ya kugombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad

“Nasikia kuna watu washapangwa na vyama vingine kuniwekea pingamizi, nawakaribisha kwa sababu kuniwekea pingamizi atakuja kutoa haja zake na ushahidi wake, na mimi naujua vilevile.

“Sioni kama kuna pingamizi yoyote kama itasimama juu yangu. Mimi nimezaliwa Mtambwe, hamjui ninyi? Ndiyo sifa ya kwanza ya mgombea urais awe Mzanzibari wa kuzaliwa sio Mzanzibari mkaribishi,” ameeleza Maalim Seif.

Kwa mujibu wa ratiba ya ZEC, zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu  za kugombea urais, lilifunguliwa tarehe 26 Agosti 2020 na linatarajiwa kufungwa leo tarehe 9 Septemba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!