Maalim Seif afungiwa kufanya kampeni

Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imemfungia siku tano kutofanya kampeni, Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kuanzia kesho 16-20 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Hatua hiyo inatokana na Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko Maalim Seif ameshawishi watu wapige kura 27 Oktoba.

Kwa maana hiyo, Maalim Seif atakuwa amebakiza siku sita za kufanya kampeni kuanzia tarehe 21 hadi 26 Oktoba 2020 na siku inayofuata itakuwa ni kura ya awali na 28 Oktoba kura kwa wananchi wote.

Kilichomkuta, Maalim Seif ni kama kilichomtokea Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema aliyefungiwa na kamati ya maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutofanya kampeni kwa siku saba.

Lissu alilalamiliwa na vyama vya NRA na CCM kwamba ametoa maneno ya uchochezi yaaiyoweza kuthibitishwa.

KAMATI ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imemfungia siku tano kutofanya kampeni, Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kuanzia kesho 16-20 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar ... (endelea). Hatua hiyo inatokana na Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko Maalim Seif ameshawishi watu wapige kura 27 Oktoba. Kwa maana hiyo, Maalim Seif atakuwa amebakiza siku sita za kufanya kampeni kuanzia tarehe 21 hadi 26 Oktoba 2020 na siku inayofuata itakuwa ni kura ya awali na 28 Oktoba kura kwa wananchi wote. Kilichomkuta, Maalim Seif ni kama kilichomtokea Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema aliyefungiwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!