Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aeleza tiba ajira za ubaguzi Z’bar
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif aeleza tiba ajira za ubaguzi Z’bar

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ameeleza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ajira ikiwa ni hatua za kutibu ubaguzi wa ajira visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Amekiri kuwepo kwa ubaguzi wa ajira kwa baadhi ya Wazanzibari, unaotokana na misingi ya tofauti za kisiasa na kwamba, tatizo hilo linakwenda kupatiwa ufumbuzi.

“… kulikuwa na changamoto katika taasisi za kiserikali katika kuajiri, sasa serikali itaanzisha mfumo rasmi wa kimtandao kwa kuomba ajira na sio kama zamani,” amesema Maalim Seif wakati wa ziara yake kisiwani Pemba jana Jumatano tarehe 6 Januari 2021.

Kwenye ziara hiyo, Maalim Seif amesema, wananchi hususan vijana, wanatarajiwa kunufaika na uwekezaji ambao uko njia kufanyika katika uvuvi.

“Kuna uwekezaji unaotarajiwa kufanyika katika sekta ya samaki, uwekezaji huu utawanufaisha hususani vijana,” amesema.

Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT –Wazalendo, anaendelea na ziara yake Pemba akikutana na viongozi mbalimbali wa serikali, chama chake na wakuu wa taasisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!