Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aanza kuwakamua sumu Wazanzibari
Habari za Siasa

Maalim Seif aanza kuwakamua sumu Wazanzibari

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Spread the love

MAALIM Self Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza athari  zinazotokana na siasa za mivutano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akiwa kwenye ziara yake katika Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 2 Oktoba 2021 amesema, mivutano ya kisiasa imekuwa ikiathiri ustawi wa Zanzibar.

Ziara yake imehusisha kukutana na wananchi wa makundi  mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali, viongozi wa dini, watu mashuhuri, wazee, Vijana na wanawake kisiwani humo.

Baada ya ukaribisho kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud,  Maalim Seif alieleza historia ya Zanzibar kabla na baada ya Uhuru.

“Sisi sote tuna maslahi mapana na hatma ya Zanzibar, na kama maslahi yakiwa mazuri sote tutanufaika, na maslahi yakiwa mabaya basi sote tutaathirika, hivyo lazima tutambue sisi ni ndugu na Zanzibar ndio nyumbani kwetu, tusishiriki kuibomoa nyumba yetu,” amesema na kuongeza:

“Wazanzibari tumepewa neema kubwa ya umoja, hata lugha yetu ya kuwasiliana ni moja ya Kiswahili, na hata dini waliowengi wanaabudu dini sawa, hii inaonesha kwamba hili ni taifa lililoshikamana, na hii ni tunu ya Taifa.

“Kwa hiyo nawasihi sana Wananchi wenzangu, asitokee mtu wa nje akaleta chokochoko na kulichafua Taifa hili, kwani gharama ya kuirudisha amani itakuwa kubwa sana.”

Maalim Seif ambaye aligombea urais visiwani humo kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, suala la ushirikiano katika nchi haliepukiki na kwamba, Zanzibar inahitaji umoja na mshikamano.

“Mpaka sasa kuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hii ni kuonesha kwamba maendeleo ya Zanzibar yataletwa na Wazanzibar wenyewe,” amesema.

Maalim Seif pia amezungumzia ushirikiano wa Serikali na Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 2010-2015.

Mfano mzuri wa mshikamano niule uliodumu kati ya mwaka 2010 mpaka 2015 ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa,  ambapo maisha ya utulivu na hali ya amani katika nchi yalionekana wazi, ila baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 mambo yaliyotokea tumeona wote namna hali ya amani na Usalama ilivyochafuka mpaka kufikia katika uchaguzi mkuu wa 2020.

“Uchaguzi huu umeacha majeraha makubwa kwa wananchi, na hii imetokea baada ya kutokuwepo mashirikiano,” amesema na kuonveza:

“…mbali na yote yaliyotokea, mimi Maalim Seif na mwenzangu Rais Husein Mwinyi, tumesafiana nia na lengo letu kwa sasa ni kujenga nchi hii, kuweka umoja na mshikamano na dhamira yetu kuu nikuipeleka nchi hii katika hatma njema kwa maslahi yetu na vizazi vyetu”.

Maalim Seif amesisitiza kwamba, suala la maendeleo litafikiwa ikiwa Katiba ya Zanzibar itafuatwa kikamilifu, na kuheshimiwa kwa kuhakikisha Wananchi wote wanapata haki sawa sambamba na kupiga vita rushwa na  ubaguzi.

Katika kukazia suala la Maendeleo, Maalim Seif  amewaelekea viongozi wa Serikali kwa kuwaambia kwamba, “Mafanikio ya Zanzibar yatakuja kwa kutenda haki sawa na uadilifu kwa Wananchi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!