Friday , 19 April 2024
Habari za Siasa

Ma-DED wala kibano

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

WAKURUGENZI wa halmashauri nchini, wameagiza kurejesha fedha walizokopa kwenye taasisi za fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 18 Novemba 2019 na Seleman Jafo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Kauli hiyo inatoka ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli, kupiga marufuku halmashauri kukopa kutoka taasisi za fedha bila idhini ya serikali.

Wakati huo huo, Jafo ameagiza halmashauri ambazo hazijaanza kutumia fedha za mikopo, kuzirejesha kwenye taasisi za fedha.

“Ambao hawajaanza kutumia mikopo hiyo, wanatakiwa kuirejesha katika taasisi hizo, wale ambao wamechukua mikopo ndani ya wiki moja na wameituma walete taarifa, ofisi itatoa maelekezo, kuanzia leo kila kitu kinasimama kuhusu mikopo,” ameagiza Jafo.

Aidha, Jafo ametoa wiki moja kwa halmashauri zenye mikopo, kuwasilisha taarifa za mikopo hiyo katika Wizara Ofisi ya Rais-TAMISEMI, na kuonya kwamba, kiongozi atakayekiuka agizo hilo na au atakayetoa taarifa za uongo kuhusu mikopo hiyo, atachukuliwa hatua.

“Ninatoa wiki moja kuanzia leo siku ya Alhamisi mpaka Jumatano ijayo, nipate ofisini kwangu taarifa za halmashauri zote zilizochukua mikopo mbalimbali katika mabenki,  je mkopo huo ulichukuliwa kiaisi gani, kwa jambo gani na riba yake ni ngapi,” amesema Jafo na kuongeza;

“Ndani ya wiki moja nipate taarifa kutoka katika halmashauro zote, na sitegemei mkurugenzi ataficha taarifa ya halmahsuri yake, kama itabainika mkurugenzi yeyote ambaye amechukua mkopo kwa halmashauri yake lakini taarifa hizo zitakaposhindwa kutufikia taarifa sahihi, kama halamshauri imechukua mkopo halafu wiki moja imekwisha mkurugenzi ahajatoa taarifa ofisi ya rais tamisemi.”

Jafo amemuagiza Eng. Joseph Nyamhanga kuwasimamia wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo mara moja.

“Nichukue fursa hii kumuagiza Injinia Nyamhanga,awasiamamie wakurugenzi wake wote, jambo hili halitavumilika tena kuanzia sasa, katibu tamisemi ahakikishe wakurugenzi wake wote hawakiuki taratibu za serikali, wanatimiza matakwa ya serikali.

Jafo amesema baada ya wizara yake kupata taarifa za mikopo ya halmashauri, itatoa maelekezo ya kufanya kwa mamlaka husika.

“Mara baada ya taarifa hiyo, ofisi itatathimini aina ya mikopo iliyochukuliwa na kutoa melekezo ya ziada, ambao hawajaitumia mikopo hawapaswi kuitumia, wanatakiwa kuirejesha,” ameeleza Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!