Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu yake

Lulu ahukumiwa jela miaka miwili, ajipanga kukata rufaa

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu Msanii wa Filamu, Elizabeth Micheal (Lulu) kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba, anaandika Faki Sosi.

Hukumu iliyosomwa na Jaji Sam Rumanyika imemtia hatiani Lulu kuwa alimuua msani mwenzake, Marehemu Kanumba bila kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 Sinza Kinondoni Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 12, 2017, lakini baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu hiyo leo.

Jaji Rumanyika anesema amemtia hatiani lulu kuuwa bila kukusudia kwa kuzingatia kifungu cha 195 cha sheria.

Upande wa Jamhuri ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba moja na marehemu na aliyekuwepo siku ya tukio, Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia hiyo ambaye aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka.

Mama mzazi wa Lulu akitoka mahakamani baada ya mtoto wake kusomewa hukumu

Wengine ni Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Kanumba pamoja askari ASP Ester aliyefanya upelelezi kwenye tukio hilo pamoja na kumtia mbaroni Lulu.

Lulu aambaye anatetewa na wakili Peter Kibatala, waliwasilisha mashahidi wa wawili ambao ni Lulu mwenyewe aliyehadithia mazingira ya tukio na kueleza kuwa hakuhusika kwa namna yoyote kwenye kifo cha Marehemu Kanumba.

Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoka mahakamani

Wakili wa Lulu, Kibatala amesema wanajipanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu Msanii wa Filamu, Elizabeth Micheal (Lulu) kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba, anaandika Faki Sosi. Hukumu iliyosomwa na Jaji Sam Rumanyika imemtia hatiani Lulu kuwa alimuua msani mwenzake, Marehemu Kanumba bila kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 Sinza Kinondoni Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 12, 2017, lakini baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu hiyo leo. Jaji…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube