Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi amtumbua Mkuu Idara ya Ardhi
Habari za Siasa

Lukuvi amtumbua Mkuu Idara ya Ardhi

Spread the love

WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemvua Ukuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Iringa, Wilbert Mtongani kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya kazi. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Lukuvi amtengaza uamuzi huo leo tarehe 2 Desemba 2019, katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi mkoani Iringa.

Mtongani anatuhumiwa kuanzisha ofisi binafsi inayoshughulikia masuala ya upimaji ardhi, ambapo Lukuvi amesema, kitendo hicho ni kuihujumu serikali inayompa mshahara kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kupitia ofisi ya umma.

 “Wapo wanaotaka huduma wanampa kwanza hela yeye halafu wanaenda ofisi za umma. Nakuvua ukuu wa idara wa manispaa kuanzia leo hufai kuwa mkuu wa idara.  Leo katibu mkuu ataleta barua ya nani anamkaimisha ukuu wa idara,” ameagiza Lukuvi.

Lukuvi ameeleza kuwa, atafanya uchunguzi kujua kiasi cha fedha ambazo Mtongani anatuhumiwa kuwatapeli wananchi kupitia ofisi yake, na kwamba akikutwa na hatia, atachukuliwa hatua ikiwemo kurudisha fedha za wananchi alizochukua.

 “Na nitafanya uchunguzi zaidi, huwezi kutumia mshahara wa rais halafu unawaibia watu wake, ninao ushahidi hata watu unaowachaji ninoa ushahidi na uliposikia nakuja umendoa hilo bango, haitasaidia kitu,” ameeleza Lukuvi.

Wakati huo huo, Lukuvi ameonya watendaji wa idara ya ardhi walioanzisha kampuni zao za upimaji ardhi, kuacha mara moja kwa kuwa hawaruhusiwi kufanya hivyo.

Lukuvi amedai kuwa, baadhi ya maafisa ardhi wanashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa pamoja na madiwani, kuwatapeli fedha wananchi wanaotaka kupimiwa ardhi.

“Watendaji wameanzisha makampuni ya upimaji wanapimisha watu ardhi kwa pesa, hairuhusiwi kama hutaki kazi hiyo acha, wapo watalaam wanaelewana na wenyeviti wa mitaa na madiwani wanaongeza gharama za upimaji,” amesema Lukuvi na kuongeza;

“Wewe ni afisa ardhi umeanzisha ofisi, jua umeletwa hapa kufanya kazi. Aliyekuleta hapa mwajiri wako fanya kazi za mwajiri wako , wale wote watumishi wanaofanya kama huyu mkuu wa ardhi nawajua nitawatangaza na nitawafukuza, bora kuwa na watu wachcache wanaowatumikia watu kuliko wenye tamaa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!