Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi abadili staili utoaji vibali vya ujenzi
Habari za Siasa

Lukuvi abadili staili utoaji vibali vya ujenzi

Spread the love

WaAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kwamba kuanzia sasa vibali vya ujenzi vitakuwa vinatolewa kila wiki na vitakuwa vinatolewa na maofisa wa serikali waliopo wilayani. Anaripoti Mwandishi Maalum, Arusha…(endelea).

Maofisa hao watakuwa wale wa mipango miji, ardhi, wapimaji na wathamini ambao ni wataalamu.

“Kulikuwa na ucheleweshaji wa utoaji vibali vya ujenzi Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo kwamba vibali vya ujenzi havitatolewa tena na kamati za madiwani.

“Kwasababu ilikuwa inachukua muda na walikuwa lazima walipwe posho, kwahiyo vibali vya ujenzi vitakuwa vinatoka kila wiki na vitatolewa na wataalamu wa serikali waliopo wilayani” amsema Lukuvi.

Amesema kwamba, Serikali imeamua kubadili utaratibu huo ili kuwawezesha wananchi ambao walikuwa wana fedha ya kujenga maeneo yao lakini vibali vya ujenzi vilikuwa havitolewi kwa wakati, na kuna watu ambao walikuwa wanakaa mwaka mzima wakisubiri vibali vya ujenzi kitendo amabacho kilichangia ujenzi holela katika miji.

Amesema, serikali imeamua kuchukua hatua hizo ili kuondoa kero kwa wananchi ambao walikuwa wanapata tabu ya urasimu uliokuwepo hapo awali, kitu ambacho kilikuwa ni kikwazo katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Waziri huyo amesikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi zaidi ya 200 wa Jiji la Arusha ambao walihudhuria katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Azimio la Arusha jijini hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!