KANGI Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amekemea uzembe wa baadhi ya askari polisi dhidi ya wahalifu wa ujambazi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Lugola ameeleza kuwa, uzembe huo ukikithiri itafikia pahala mamlaka husika zitaanza kuchukulia hatua maiti, za askari polisi atakaye zembea katika kupambana na wahalifu wa ujambazi.
“ Jambazi ambaye anakutana na Polisi kabla hajajiandaa kuwawahi Polisi, tayari awe amewahiwa zamani na kuangushwa chini. Na ninasema, Polisi ambaye atazembea zembea mpaka akawahiwa wakati na yeye ana mashine yake, tutafika pahala hata maiti sasa tuanze kuichukulia hatua,” amesema Lugola.
Lugola amesema kushughulika na majambazi sio sawa na kutongoza mwanamke, na kwamba lazima Polisi wawahi majambazi kabla hawajadhuru wananchi au wao wenyewe.
“Kushughulika na majambazi sio sawa na tunavyotongoza mwanamke. Unajua dada nakumaindi, unajua dada ulinipa namba ya bajaji. Hakuna, nimesema jambazi ambaye anakwenda kufanya ujambazi awahiwe kabla ya huyo jambazi hajamuwahi mwananchi,” amesema Lugola.
ReplyForward |
Leave a comment