Rais Jakaya Kikwete (kushoto) alipokuwa anamnadi Edward Lowassa jimboni kwake Monduli 2010

Lowassa kumshitaki Kikwete

WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
 
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki zinasema, Lowassa amepanga kukutana na waandishi wa habari, Jumatatu au Jumanne wiki hii.
 
Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”
 
Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake binafsi.
 
“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na kiongozi huyo.
 
Hakuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.
 
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, madiwani 20 kutoka jimboni kwake Monduli, walitangaza kukihama CCM na kujiunga na Chadema; jambo ambalo linadaiwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni maandalizi ya mwanasiasa huyo kukimbilia Chadema.
WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).   Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki zinasema, Lowassa amepanga kukutana na waandishi wa habari, Jumatatu au Jumanne wiki hii.   Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”   Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake binafsi.   “Ni kweli kwamba…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Saed Kubenea

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube