Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa amnadi mwanae Monduli, amtumia ujumbe Magufuli
Habari za Siasa

Lowassa amnadi mwanae Monduli, amtumia ujumbe Magufuli

Edward Lowassa
Spread the love

EDWARD Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani nchini Tanzania, amemtumia ujumbe mgombea urais wan chi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli kuelekea Uchaguzi  Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Monduli … (endelea).

Lowassa ametuma salamu hizo jana Jumatano tarehe 2 Septemba 2020, katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Barafu uliopo Kata ya Mto wa Mbu alipokuwa akimnadi mwanae, Fredrick anayegombea Ubunge Monduli jijini Arusha.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alimtuma, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu akamwambie Rais Magufuli kwamba kuna zawadi yake ya kura kutoka kwa wananchi wa Monduli na Tanzania kwa ujumla.

“Majaliwa ukienda mwambie Rais Magufuli kuna zawadi moja tu ya kura kutoka kwa WanaMonduli,” alisema Lowassa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa wakati alipozindua kampeni za CCM wilayani Monduli

Lowassa aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) alisema, Magufuli anapaswa kupigiwa kura kutokana na kazi nzuri aliyofanya.

“Nimuombee kura Rais Magufuli, ametuongoza katika muda wa miaka mitano, amefanya maajabu sana. Nataka niseme moja tu, ni kiongozi wa ajabu hapa duniani. Tuongozaneni kupiga kura, mumchague pamoja na wagombea wa CCM,” amesema Lowassa.

Wakati huo huo, Lowassa amemuombea kura Fredrick, akiwataka WanaMonduli kumchagua siku ya kupiga kura.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM wilayani Monduli

Naye Waziri Majaliwa amemuombea kura Rais Magufuli pamoja na Fredrick.

“Leo niko mbele yenu kwa kazi moja tu, kuomba kura Watanzania wote na wanaMonduli, naomba kura za WanaCCM wote bila kujali vyama vyenu mumpigie kura Rais Magufuli na Fredrick Lowassa,” amesema Majaliwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Fredrick ameomba kura akiahidi kushughulikia tatizo la migogoro ya ardhi.

“Migogoro ya ardhi ni jambo kubwa sana, kama tunavyofahamu ardhi haiongezeki bali sisi tunaongezeka, migogoro ikizidi inaleta chuki. Nitaenda kuitatua,” amesema Lowassa aliyewahi kuliongoza jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 15.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!