Saudi Arabia

‘Lockdown’ siku ya Eid

Spread the love

SIKU ya Sikukuu ya Eid el Fitr na siku nne mbele, wananchi wa Saudi Arabia wametangaziwa kutotoka nje. Utekelezaji wa tangazo hilo utaanzia tarehe 23 mpaka 27 Mei 2020. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).  

Hatua hiyo imechukuliwa ili kuzia maambukizo mapya ya virusi vya corona (COVID-19), na kwamba watu hawatoruhusiwa kutoka nje kwa saa 24 katika siku zote tano.

Mpaka leo Jumatano tarehe 13 Mei 2020, taifa hilo lina maambukizo 42,925 vifo vikiwa 264 huku waliopona wakiwa 15,257.

Taarifa ya Suleyman Soylu, Waziri ya Mambo ya Ndani ya taifa hilo imeeleza, mpaka sasa biashara na shughuli zingine kwenye maeneo mbalimbali ya taifa hilo yanaendelea kama kawaida lakini kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni.

Wizara hiyo imesisitiza, pamoja na maeneo hayo kuwa huru kwa muda huo, wakazi wa Mji wa Makka wanaendelea kuwa ndani mpaka hapo tangazo lingine litapotolewa.

Makka ndio mji pekee katika taifa hilo uliofungwa, watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani.

SIKU ya Sikukuu ya Eid el Fitr na siku nne mbele, wananchi wa Saudi Arabia wametangaziwa kutotoka nje. Utekelezaji wa tangazo hilo utaanzia tarehe 23 mpaka 27 Mei 2020. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).   Hatua hiyo imechukuliwa ili kuzia maambukizo mapya ya virusi vya corona (COVID-19), na kwamba watu hawatoruhusiwa kutoka nje kwa saa 24 katika siku zote tano. Mpaka leo Jumatano tarehe 13 Mei 2020, taifa hilo lina maambukizo 42,925 vifo vikiwa 264 huku waliopona wakiwa 15,257. Taarifa ya Suleyman Soylu, Waziri ya Mambo ya Ndani ya taifa hilo imeeleza, mpaka sasa biashara na shughuli zingine kwenye maeneo mbalimbali…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!