Lijualikali aondoka Chadema, amwaga chozi kwa kunyanyaswa

Spread the love

MBUNGE wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, amejiondoa katika chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni Mjini Dodoma jioni ya leo, Lijualikali amesema, ameamua kuondoka Chadema kwa kuwa chama hicho, kinaendeshwa “kidikteta.”

Amesema, uamuzi wa chama chake kususuia mkutano wa Bunge kwa madai ya kujitenga na karatini, haukufuata taratibu.

Akiongea kwa uchungu huku akitokwa na machozi, Lijualikali amesema, amepitia makubwa na kwamba hawezi kubaki Chadema, kwa kuwa kuna mambo ya ajabu sana.

Amesema, wabunge wa Chadema wametawaliwa na woga, na hivyo kushindwa kumwambia kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa unakosea.

Amemtuhumu Mbowe kutafuna baadhi ya fedha za chama hicho na kuongeza kuwa kila wanapotaka kuuliza, wanaambiwa hakuna kuhoji.

“Niko tayari kulima hata mpunga, kuendesha bodaboda na kufanya kazi nyingine yeyote. Niko tayari, lakini siko tayari kubaki Chadema,” ameeleza.

Lijualikali amesema yuko tayari kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) endapo kitakubali kumpokea na atakuwa tayari kufanya kazi yoyote ndani ya chama hicho

MBUNGE wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, amejiondoa katika chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma ... (endelea). Akizungumza bungeni Mjini Dodoma jioni ya leo, Lijualikali amesema, ameamua kuondoka Chadema kwa kuwa chama hicho, kinaendeshwa "kidikteta." Amesema, uamuzi wa chama chake kususuia mkutano wa Bunge kwa madai ya kujitenga na karatini, haukufuata taratibu. Akiongea kwa uchungu huku akitokwa na machozi, Lijualikali amesema, amepitia makubwa na kwamba hawezi kubaki Chadema, kwa kuwa kuna mambo ya ajabu sana. Amesema, wabunge wa Chadema wametawaliwa na woga, na hivyo kushindwa kumwambia kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa unakosea. Amemtuhumu Mbowe kutafuna baadhi ya fedha za…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!