January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Liverpool waongoza kinyang’anyiro Tuzo za FIFA

Spread the love

KLABU ya Liverpool inayoshriki Ligi Kuu England imetoa wachezaji wanne kati ya 11 waliopo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa Dunia 2020 zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Liverpool ambao walifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu nchini England mara baada ya miaka 30, pia wamefanikiwa kutoa kocha mkuu wa kikosi hiko Jurgen Klopp kuwa kati ya wanaowania tuzo ya kocha bora.

Wachezaji hao waliopo kwenye kinyang’anyiro hiko ni beki wa kati Virgil Van dijk, Mohamed Salah, Sadio Mane na kiungo Thiago Alcantara ambaye alijiunga na timu hiyo katika dirisha kubwa la usajili akitokea klabu ya Buyern Munchen ya nchini Ujerumani.

Licha ya wakali hao kutoka Liverpool wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo, Kevin De Bruyne, Robert Lewandowski, Kylian Mbappe, Lionel Messi, Neymar na Sergio Ramos.

Tuzo hiyo ambayo 2019 ilienda kwa mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi mara baada ya kuwashinda beki wa Liverpool Virgil Van Dijk na mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo.

Tuzo hizo ambazo ni namba moja kwa ukubwa dunia zitafanyika Alhamisi tarehe 17 Desemba, 2020 ambapo zitamtangaza kinara sambamba na kikosi cha wachezaji 11 bora wa dunia kwa mwaka 2020.

error: Content is protected !!