Salum Mwalimu, Mgombea Mwenza wa Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema

‘Lissu ndiye amiri jeshi mkuu ajaye’

Spread the love

SALUM Mwalimu, mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ndiye amir jeshi mkuu ajaye. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

 Amesema, Lissu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, anakwenda kumshinda kwa kura nyingi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni katika Viwanja vya Shujaa, Morogoro tarehe 29 Septemba 2020 amesema, watumishi wa umma na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji wajiandaye kisaikolojia kuongozwa na Chadema.

“Chadema hatuji na askari wetu, hatuna wanajeshi wetu wala watumishi wa umma tuliowaweka pembeni, tunakuja kutumia watumishi, jeshi haohao, kinachokwenda kubadilika ni jambo moja tu, kila aliyepo kwenye nafasi yake ahakikishe anatenda haki na kutoa uhuru kwa raia tunaokwenda kuwaongoza,” amesema.

Pia amesema tayari wamempa taarifa Dk. Magufuli kwamba hawana kinyongo naye, bali watamtunzia heshima yake kama Rais Mstaafu.

SALUM Mwalimu, mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ndiye amir jeshi mkuu ajaye. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).  Amesema, Lissu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, anakwenda kumshinda kwa kura nyingi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli. Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni katika Viwanja vya Shujaa, Morogoro tarehe 29 Septemba 2020 amesema, watumishi wa umma na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji wajiandaye kisaikolojia kuongozwa na Chadema. “Chadema hatuji na askari wetu, hatuna wanajeshi wetu wala watumishi wa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Christina Haule

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!