Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu mbaroni tena, apanga kugoma kula
Habari za SiasaTangulizi

Lissu mbaroni tena, apanga kugoma kula

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipokuwa anashikiriwa na Kituo Kituu cha Polisi Dar es Salaam.
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo ikiwa ni dakika chache baada ya kufutiwa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili, anaandika Charles William.

Lissu amekamatwa akiwa ndani ya Mahakama ya Kisutu ambapo hii leo mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kufuta kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili baada ya serikali kuwasilisha taarifa kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.

“Nimekamatiwa Mahakamani Kisutu. Sikutoka hata nje ya mahakama nikakamatwa tena. Wamenipeleka Central kwa mahojiano, polisi walionikamata wamekataa kuniambia wananikamata kwa kosa gani,” amesema Lissu katika taarifa aliyoandika na kusambaza akiwa mikononi mwa polisi.

Lissu amedai kuwa, anaamini kukamatwa kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja uchaguzi ujao wa Chama cha Mawakili hapa nchini (TLS), unaotarajia kufanyika wiki mbili zijazo.

“Serikali hii, kwa kutumia mawakili wao vibaraka, imekuwa na mkakati mkubwa wa kunizuia kugombea urais wa TLS. Walipanga kwenda kupinga kugombea kwangu mahakamani. Tumewasema hadharani na kuzianika njama zao. Sasa wameamua kutumia rungu lao la siku zote.

“Hofu yao ni kubwa sana. Natabiri watataka kuniweka ndani hadi baada ya uchaguzi huo. Mawakili vibaraka wao wataleta hoja kwenye TLS kwamba mgombea asiyekuwapo ukumbini wakati wa Uchaguzi aondolewe kwenye kinyang’anyiro hicho,” ameandika.

Lissu ameeleza kuwa hakuna makatazo yoyote katika kanuni za uchaguzi yanayozuia mgombea kuondolewa kwenye uchaguzi kwasababu tu hayupo ukumbini na amewataka mawakili washikilie msimamo kwamba wote walioteuliwa kugombea wapigiwe kura.

“Nimekamatwa asubuhi na mapema. Hakuna sababu ya kutokunipeleka mahakamani leo. Kama hawatanipeleka mahakamani, nitaanza mgomo wa kula chakula, sitakula hadi nitakapopelekwa mahakamani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!