Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu, Magufuli kukutana Kigoma
Habari za Siasa

Lissu, Magufuli kukutana Kigoma

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema watakuwa Mkoa mmoja wa Kigoma na Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Wawili hao ambao wote ni wagombea urais wanakutana leo Jumamosi tarehe 19 Septemba 2020 kwa kila mmoja akiwa na shughuli yake.

Jana Ijumaa, Rais Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Chama Mapinduzi (CCM) alikuwa na mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Lissu alifanya mikutano majimbo kadhaa ya Rukwa na Katavi.

Leo Jumamosi, ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha Lissu atakuwa Mpanda Mjini mkoani katavi asubuhi kisha ataingia Kigoma akianza na Jimbo la Kigoma Kaskazini atakwenda Kalimi, Buhigwe na atamalizia mkutano Kigoma Mjini saa 10 jioni.

Ratiba hiyo hiyo inaonyesha, mgombea urais wa CCM, Rais John Magufuli Uvinza Mkoa wa Kigoma kisha ataingia Mkoa wa Tabora majimbo ya Kaliua na Urambo.

Hata hivyo, Rais Magufuli bado yuko mkoani Kigoma kwa shughuli ya kiserikali iliyoanza asubuhi kwa kumpokea Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye aliyefanya ziara ya siku moja.

Rais Ndayishimiye amewasilia Kigoma na kupokelewa na Rais Magufuli Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo wamezungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza uwanjani hapo kisha kwenda kuzindua Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma na baadaye kwenda kuzungumza Ikulu ndogo mkoani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!