Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu kuzindua kampeni leo Dar
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu kuzindua kampeni leo Dar

Tundu Lissu, mgombea wa Urais wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, atazindua kampeni zake za uchaguzi mkuu kesho Ijumaa 28 Agosti 2020 jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ratiba iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema inaonyesha Lissu na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu watatumia siku tatu jijini Dar es Salaam.

Wakati Chadema wakizinduliwa kampeni zao Dar es Salaam, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli yeye anazinduliwa kampeni Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020.

Kampeni za uchaguzi mkuu zimeanza kuanzia tarehe 26 Agosti na zitahitimishwa 27 Oktoba na siku inayofuatia ya Jumatano 28 Oktoba 2020 itakuwa ni ya uchaguzi mkuu.

Taarifa ya Makene imesema, kesho Ijumaa kampeni zitazinduliwa katika Uwanja wa Zakhiem Mbagala, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020, Lissu atakuwa Uwanja wa Tanganyika Parkers, jijini Dar es Salaam na Jumapili kampeni hizo zitakuwa uwanja wa Tabata Shule ya Msingi, Segerea, jijini Dar es Salaam.

Fuatilia ratiba itakavyokuwa baada ya kutoka Dar es Salaam;

  • 31 Agosti, 2020, Uwanja wa Relini, jijini Arusha, kuanzia saa 400 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 1 Sepetemba 2020, Uwanja wa Furahisha, Kitangili, jijini Mwanza, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 2 Septemba 2020, Uwanja wa Lubaga joshoni, Manispaa ya Shinyanga, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 3 Septemba 2020, Uwanja wa Chipukizi, Tabora mjini, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 4 Septemba 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 5 Septemba 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 6 Septemba 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
  • 7 Septemba 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!