Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kuvuliwa Ubunge: Chadema yabadili gia angani
Habari za SiasaTangulizi

Lissu kuvuliwa Ubunge: Chadema yabadili gia angani

Spread the love

HATUA ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kumvua ubunge Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki siku mbili zilizopita, kumejibiwa vikali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Pamoja na kulaani hatua hiyo, Chadema imeeleza kwenda kortini kumpinga Spika Ndugai ikiwa ni pamoja na kuiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akizungumia kadhia hiyo Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, Spika Ndugai amesitisha ubunge wa Lissu ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kinyume na utaratibu.

Ijumaa ya terehe 28 Juni 2019 katika Kikao cha 15 katika  Bunge la 11 jijini Dodoma, Spika Ndugai alitoa kauli ya kusitisha ubunge wa Lissu kwa madai ameshindwa kuhudhuria vikao na mikutano ya Bunge kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa sasa Lissu yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu, baada ya kushambuliwa kwa risasi tarehe 7 Septemba 2017 na watu waanaotajwa na serikali kuwa ‘wasiojulikana.’

Awali, baada ya kushambuliwa nyumbani kwake Area ‘D’ wakati akitoka kwenye shughuli za vikao bungeni, Lissu alipelekwa Nairobi, Kenya kwa matibabu ya awali na baadaye alipelekwa Ubelgiji.

Akiwa Kenya, Samia Suluhu Hassan ambaye ni Makamu wa Rais alimtembelea Lissu na kumpa salamu kutoka kwa Rais John Magufuli.

Akizungumzia uamuzi wa kwenda mahakamani Dk. Mashinji amesema, chama hicho kinakwenda kuomba tafsiri ya matumizi ya sharia iliyotumiwa na Spika Ndugai kutengua ubunge wa Lissu.

Kiongozi huyo mbele ya wanahabari leo tarehe 30 Juni 2019 amesema, chama hicho kimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Bunge, kuomba nakala ya uamuzi huo sambamba na kuiandika barua NEC.

“Tunapozungumza na ninyi muda huu, ni siku ya tatu tangu toka spika alipoitangazia dunia kuwa Lissu amekoma kuwa Mbunge. zimetolewa sababau kuu mbili, moja wapo ni utoro na katika utoro huo Spika alieleza kuwa, hajui Lissu yupo wapi, hajui yupo bungeni Dodoma  au yupo wapi?

“Na sababu ya pili ni Lissu kutowasilisha tamko la mali zake kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kwamba, Spika ameshamuandika Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa Jimbo la Lissu lipo wazi,” amesema Dk. Mashinji.

Akituhumu hoja hizo amesema, Spika Ndugai amekosa hoja za kuzima ubunge wa Lissu ambapo amedai amesema ni uongo. “Si kweli kwamba hajui Lissu alipo,” amesema na kuongeza:

“Lissu hakai huko kwa vile anapenda, sidhani kuna mtu anapenda kukaa Hospitali isipokuwa kuwe na muito wa asili ugonjwa, na Lissu ni mgonjwa na utaratibu wa matibabu ya mgonjwa anaujua daktari wake.”

Dk. Mashinji ameeleza kushangazwa na hatua ya Spika Ndugai kueleza kuwa hajui alipo kwa maelezo kuwa, baada ya mbunge hujeruhiwa, alikuwa mstari wa mbele kumsaidia.

“Pia aliwahi kueleza atakwenda Lissu popote alipo, aidha Nairobi au popote duniani,” amesema Dk. Mashinji.

Amesema kuwa, yapo mawasiliano rasmi kati ya Ofisi ya Bunge na Lissu akitoa mgogoro ulioibuliwa hivi karibuni kuhusu mshahara wa Lissu.

Katibu mkuu huyo amesema, Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma haikumuita Lissu ili kumuhoji juu ya mali zake.

Na kwamba, kinachofanywa na Spika ndugai ni kudanganya umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!